Wednesday 8 November 2017
Friday 21 July 2017
Tuesday 14 February 2017
UCHUMI NA MKRISTO by ALEX JOHN WAMBI. MWALIMU WA FPCT CHAMWINO DODOMA.
06:16:00
No comments
UCHUMI NA MKRISTO
SI
MAPENZI YA MUNGU TUWE NA MAISHA DUNI/ MASKINI
Napenda kuanza
kukuambia ya kuwa si mapenzi ya Mungu uwe maskini. Kwa sababu tangu kuwekwa
misingi ya ulimwengu huu, Mungu hakupanga kuwa watu wake aliowaumba wawe
maskini; bila kujali rangi, kabila, wala taifa. ( Kumbuka EFESO 3:20;)
Mtu
maskini maana yake ni mtu mhitaji. Mtu aliye maskini wa
mambo ya mwili ni yule aliye mhitaji wa mambo ya mwili. Na mambo ya mwilini
ninayoyasema ni mavazi, chakula na mahali pa kulala. Yesu Kristo hakusema heri
wale walio na mahitaji ya chakula, mavazi, afya na malazi.
Japo ni
imeandikwa katika Mithali 22:2, kuwa “Tajiri na maskini hukutana pamoja;
Bwana ndiye aliyewaumba wote”. Lakini fahamu ya kuwa ingawa matajiri na maskini
waliopo wote waliumbwa na Mungu; tangu mwanzo wa uumbaji Mungu hakuyaweka
matabaka haya mawili.
SABABU 4 KWA
NINI SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASIKINI.
- Mungu
ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri
“ Bali utamkumbuka Bwana , Mungu wako,
maana ndiye akupaye NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; ili alifanye
imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo” (Kumb. 8:18).
Lakini fahamu ya kuwa si matajiri wote waliopo duniani
wameupata utajiri kutokana na nguvu walizopewa na Mungu. Wengi wamepata utajiri
kwa njia ya dhuluma. Na ndiyo maana sehemu nyingi katika Biblia matajiri wa
jinsi hiyo wamekemewa. Soma Amosi 5:11, 12. Kwa sababu hii Mungu hayuko upande
wa matajiri hawa. Hii pia haimaanishi kuwa Mungu yuko upande wa KILA
maskini aliopo duniani. La hasha! Mungu yuko upande wa yule ayafanyaye mapenzi
yake awe tajiri au maskini (Mathayo 7:21)
- Mungu
ndiye atufundishaye kupata faida
Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo
Yesu si Mungu wa hasara bali Mungu wa faida. Imeandikwa hivi; “ Bwana, Mkombozi wako, Mtakatifu wa
Israeli, asema hivi;Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye
ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuifuata” (Isaya
48:17).
- Vitu
vyote vyema ni mali ya Bwana, na vyote vya Bwana ni vyetu ndani ya Kristo
Katika Zaburi 24:1 imeandikwa;“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya
Bwana; Dunia na wote wakaao ndani yake”
Na pia ukisoma katika Hagai 2:8 unaona imeandikwa hivi “Fedha ni mali yangu, na
dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi”
- Yesu
Kristo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri
“ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi
alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi
mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” (2 Wakorintho 8:9).
Je! unafahamu kwa nini
Yesu Kristo aliamua kuwa maskini? Ni “…….. ili kwamba ninyi mpate kuwa MATAJIRI
kwa umaskini wake”.
Najua kuna wengine watashangaa
kuusoma mstari huu; lakini ndivyo ilivyo. YESU ansema Na ndiyo maana alisema
katika Luka 4:18a ya kuwa; “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia
mafuta kuwahubiri MASKINI habari njema.”
Mtume Petro naye aliwahi kusumbuliwa sana na jambo
hili, hata ikabidi amuulize Bwana Yesu.
“Ndipo
Petro akajibu, akamwambia, tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata, TUTAPATA
NINI BASI?” (Mathayo 19:27)
“Yesu akasema, Amini, nawaambiaeni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu
waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili
yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa MARA MIA SASA WAKATI HUU, nyumba, na
ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia;
na katika ulimwengu ujao uzima wa milele” (Marko 10:29,30).
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa
maarifa ……." (Hosea 4:6). Maneno haya yaliyosemwa na
Mungu kwa kinywa cha Nabii Hosea yana ukweli ndani yake hata hivi leo. Watu
wengi sana siku hizi wanaangamizwa, wanadhulumiwa, wanahuzunishwa na maisha kwa
sababu tu wamekosa kuyajua maarifa ya Mungu yaliyomo katika Neno lake.
Tulikuwa tunafurahi tunaposoma mstari kama ufuatao; "
…..vyote ni vyenu …. Vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni
vyenu, nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu" (Wakorintho
3:21,22). Tulikuwa tunafurahi kwa kuwa maneno haya yanatupa uhalali wa kumiliki
vitu vilivyo vya Mungu. Kwa mfano Hagai 2:8 inasema "Fedha ni mali
yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa Majeshi." Pia, Zaburi
24:1 inasema "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana …"
Lakini jambo lililotusumbua ni kwamba ingawa mistari hiyo ilitupa umilikaji juu
ya fedha, dhahabu na vyote viijazavyo nchi ili tuvitumie – SISI HATUKUWA NAVYO
WALA HATUKUJUA TUTAVIPATAJE!
Tulitamani sana kuona maneno ya Wafilipi 4:19
yanatimia kwetu – nayo yanasema hivi;
"Na Mungu wangu atawajazeni kila
mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo
Yesu".
·
Lakini mnaweza kushinda kwa kusimama katika Neno langu ambalo ni upanga wa Roho
mikononi mwenu.
·
Nimesema katika Yoshua 1:8 ya kuwa mtafanikiwa ikiwa mambo matatu yatafanyika
juu ya Neno langu:
(a) Lisiondoke kinywani mwenu
(b) Mlitafakari wakati wote
(c) Na kudumu kulitenda
Ahsante,
KANUNI
ZA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA KWA
MWAMINI/MKRISTO:
usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako na
kuukuza uzalishaji wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini
kama una usimamzi mbaya wa fedha uchumi wako utayumba tu.Matatizo mengi
ya kifedha tunakimbilia kuombewa na kukemea,lakini hayo yote bila
kujifunza usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika mzizi.hata
ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha matatizo ya kifedha yatarudi baada ya muda
mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi kanuni za fedha.
1: JIFUNZE
KUWEKA NA KUWEKEZA AKIBA USILE
KILA KITU UPATAPO TOKA KWA BWANA!
Kosa
Kubwa Wanalofanya Wana Wa Mungu, Hasa Wale Waliookoka, Wanaoishi Kwa Imani, Ni
Kutojua Kuwa Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Ndani Ya Muda Maalumu, Na Hurudi
Kutupa Tena Baada Ya Muda, Na Sio Kwamba Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Kila
Siku… Hii Naizungumzia Kwenye Maeneo Ya Mahitaji Yetu Ya Kifedha, Chakula,
Vyakula, Mavazi Nk… Mungu Anapokupa Kitu, Mahitaji Yako, Huwa Anakupa NA ZIADA,
Hakupi Kipimo Cha Kula Au Kutumia Muda Ule Tu… Huwa Anatoa NA CHA ZIADA AU
NYONGEZA JUU… Lengo Kubwa La Mungu Kukupa KITU CHA ZAIDI AU ZIADA Ni Ili
Akusaidie Kwenye KESHO YAKO (Future)… Narudia Tena, Mungu Huwa Anatupa Na
Ziada, Lengo Lake Kubwa Ni Kufidia MUDA ULIOPO KATIKATI HAPA Kati Ya Pale
Alipokupa Hadi Pale Atakaporudi Tena Kukupatia Tena! MWANZO 41:25-35,48,49.
NDIO MAANA Mungu Anatufundisha Habari Za Chungu, Wasio
Na Msimamizi Wala Kiongozi Ambao Wakati Wa MAVUNO Hawali Chakula Chote Bali
HUJIWEKEA AKIBA Inayowasaidia Wakati Wa UKAME NA NJAA MITHALI 6:6-8 NA 30:24-25…
Lakini Pia Mara Nyingi Kwenye NENO LAKE, Mungu
Amezungumza Kuhusu GHALA… Ambayo Ni Sehemu Ya Kuhifadhia Au Kutunzia MAVUNO/
ULICHOPATA Kwa Ajili Ya KESHO YAKO… Pia Mungu Mara Nyingi Amesema Kuhusu
HAZINA… Inayomaanisha SHEHENA ILIYOHIFADHIWA Kwa Ajili Ya MATUMIZI YA BAADAYE…
Na Mara Nyingi Mungu Anapokuja KUTUBARIKI, Huwa Analenga HAZINA NA GHALA ZETU…
Utamsikia Akisema, “Nipate KUZIJAZA HAZINA NA GHALA ZENU” (Malaki 3:10).
Lakini Hata Yesu Mwenyewe Alijua Kanuni Hii Na Aliitendea Kazi… Hata Wakati
Alipowalisha Wale Wanaume 5000, Wanawake Wengi Na Watoto, BADO YEYE NA TIMU
YAKE WALIKUSANYA CHAKULA KILICHOBAKI
(Marko 6:42-43, Yohana 6:12-13)
YESU Alikuwa Na Uelewa Wa Kutosha Kuhusu
Mungu, Baba Yake Ya Kuwa Huwa Anatoa ZIADA, Lakini Usipoitunza Na KUTUMIA KILA
ULICHOPATA, BILA KUWEKA AKIBA, Kuna Muda Unakuja Ambao Utakuwa Na Uhitaji Na
Hata Ukimlilia Na Kumwita Mungu, HATAKUJIBU AU KUKUPA Kingine Mpaka Muda Ule
Aliopanga Utakapofika!
Mungu Anapokufungulia MLANGO Wa Kupata MSHAHARA, Au
Kipato Kizuri Kwenye Biashara Au Shughuli Zako Za Uzalishaji, USITUMIE KILA
ULICHOPATA… JIWEKEE AKIBA… WEKA GHALANI Kwa Ajili Ya Kesho Yako Au Itumie Ile
Ziada Kwa Ajili Ya KUZALISHA FAIDA ZAIDI [WEKEZA ILE ZIADA] Kwenye shughuli Au
Jambo Litakalokupa Zaidi Ya Ile Na Kukuvusha Kipindi Cha UGUMU Kitakapokuja!
Jifunze Kuweka Akiba… Lakini Mara Baada Ya Kupata Hiyo Akiba, Iwekeze Mahali
Ambapo Unaweza Kuiongeza Ili Uwe SALAMA Wakati Wenzako Watakopokuwa WANALIA
NJAA
2.
TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA NA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA
Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza kukusaidia
katika kuandaa bajeti yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari ndogo na anza
kuweka kumbukumbu za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini itakusaidi
kwa mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa
usafiri?simu?chakula?matibabu?chakula n.k ni lazima ujue wapi fedha yako
inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina mililki nini, nina nini,
nina daiwa,natuamiaje (MITHALI 27:23-24,
23:23,)
3.
JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU, KWA NANI NA KWA UTARATIBU.
(Mithali 11:24-25).kanuni ya uchumi wa Kimungu ni
tofauti,kadiri unavyotoa na sivyo unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako
unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa kwaajili ya kuwabariki wengine,kutoa kwaajili ya
wahitaji(Mithali 28:27 Mithali 11:25.Mithali 19:17,Mithali 3:9-10),Kutoa
kunafungua Baraka za Mungu katika Maisha yako.
(A) tumia fedha yako
kwa hekima na ridhika na ulicho nacho:
Zingatia vipaumbele
na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila mpangilio,manunuzi ya papo kwa
papo,usifanye matumizi yaliyo nje,yanayozidi kipato chako au uwezo wako wa
kifedha.Jifunze kuridhika na kuuepuka tamaa.usifuje fedha kwa matumizi ya
ovyo.jifunze kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9)
Alex John Wambi,
Mwalim,FPCT Chamwino.
Sunday 12 February 2017
KUOKOKA-KIPEPERUSHI KILICHOANDALIWA KWA AJILI YA USHUDIAJI.
12:27:00
No comments
1.
MAANA YA KUOKOKA
Kuokoka ni kitendo cha kuzaliwa m
ara ya pili yaani kuzaliwa kwa
roho.
YOHANA 1:12-13 “ bali wote
waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Ndio wale waliaminio
jina lake(YESU). Wamezaliwa si kwa damu(ukoo), si kwa mapenzi ya mwili wala kwa
mapenzi ya mtu(vikao) bali kwa mapenzi ya Mungu.
Wokovu ni neema na mapenzi ya
Mungu tu na si vinginevyo, si kwa ajili ya kumfurahisha aliye kushuhudia neno,
mhubiri, mzazi, dhehebu, dini au kabila Fulani.
WAEFESO 2 : 8, 9 “kwa maana
mmeokolewa kwa neeema kwa njia ya imani ambayo haikutokana na nafsi zenu, ni
kipawa(uwezoau nguvu ) cha Mungu.
Msitari wa tisa(9) “ si kwa matendo (wema au uzuri au elimu au mali au kimo
chako ) mtu awaye yote asije akajisifu” yaani asiwe na kiburi kwa sababu
AMEOKOKA.
Kuokoka ni kupata sifa ya kuingia
katika ufalme wa Mungu. YOHANA 3: 5-6 “mtu asipozaliwa kwa maji(ubatizo wa maji
mengi) na kwa ROHO(IMANI) hawezi kuingia katika ufalme w Mungu.
KUOKOKA ni kufanywa upya baada ya
kuuvua utu wa kale au mwenendo( tabia) WAEFESO 4:22-24 ‘vueni kwa habari ya
mwenndo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kuzifuata tama zidanganyazo
mfanywe upya, mkavae utu upya ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na
utakatifu wa kweli.
2.
HATUA MBILI ZA KUCHUKUA WAKATI WA
KUOKOKA
WARUMI 10: 9-10
(i)
KUKIRI;-
Ukimkiri(kutamka) kwa kinywa chako yakuwa YESU kristo ni BWANA
na mwokozi wa maisha yako UTAOKOKA.
(ii)
KUAMINI;- Ukiamini kuwa MUNGU alimleta
yesu duniani akazaliwa, akafa kwa ajili ya dhambi zako na akafufuka kutoka
katika wafu UTAOKOKA.
3.
KWA NINI TUNAOKOLEWA KWA NJIA YA
IMANI?
(I)
Kwa
sababu lazima ubadili imani yako iliyojengwa katika mizimu, uganga, upagani,
uchawi, uisramu, matambiko, kafara n.k. sas umwamini MUNGU wa miungu na Bwana
wa mabwana ambaye imani ktika yeye imejengw katika neno lake . WARUMI 10:17-
“basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo(YESU)
(II)
Kwa
sababu pasipo imani haiwezekani kumpendeza MUNGU,
WAEBRANIA
11:6 –“ pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila
amwendeaye(anyetaka kuwa mtoto MUNGU) lazima aamini ya kwamba MUNGU yupo na
kwamba huwapa thawabu(Baraka, kibali, majibu) wale wamtafutao”
4.
MAMBO MHIMU YA KKUZINGATIA BAADA
YA KUOKOKA.
(a)
Wokovu
unapatikana kwa YESU pekee, si katika dini au mtume au nabii au dhehebu lolote.
Usianganyike.
MATENDO 4:12. Toba ndio njia pekee yakumrud ia
na kutengeneza na MUNGU na kutafuta
amani. MATENDO 3:19, 1YOHANA 1:8-9( kwa toba tunapata ondoleo la dhambi)
(b)
Epuka
tama zipinganazo na roho na jitahidi kutenda mema. 1PETRO 2 : 11-12, zingatia
sana YAKOBO 4: 17 biblia inasema “ yeye
ajuaye kutanda mema na wala hayatendi
kwake huyo ni dhambi”.
(c)
Mtii
MUNGU daima na mpinge shetani mara zote yeye pamoja na ushawishi wake wote. YAKOBO
4:7 “ basi mtiini MUNGU mpingeni shetani, mkalibieni MUNGU nae atawakaribia
ninyi.
(d)
Kaa
ndani ya YESU ili upate kuzaa sana, kustawi, kufanikiwa. YOHANA 15:1-17.
(e)
Tafuta
kanisa la watu waliookoka ili ukamwabudu MUNGU
huko, ili ukue kuroho. MATENDO 2:4-42
ishi
kwa kumaanisha maisha ya wokovu(kubali kubadilika, kubali kubatizwa na
kujifunza neno ili uwe mwanafunzi wa yesu. MATHAYO 28:19-20.
SALA YA TOBA
“BWANA YESU nakiri mimi ni mwenye dhambi,
naomba unisamehe dhambi zote nilizozitenda kwanza kwa maneno na kwa matendo
unitakase kwa damu yako, karibu moyoni mwangu, uwe BWANA NA MWOKOZI wa maisha yangu, naomba ufute jina langu
katika kitabu cha hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima, wewe shetani
kuanzia leo! Ninakukataa na kazi zako zote, BWANA YESU naomba ROHO mtakatfu
anisaidie kuishi maisha matakatifu, kwa jina la YESU Kristo naamini NIMEOKOKA
AMENI!
posted by MR. BOAZ ELIYA,
edited by evanglism departiment
cooperating with EV. DASTAN
posted by MR. BOAZ ELIYA,
edited by evanglism departiment
cooperating with EV. DASTAN
Wednesday 18 January 2017
SEMINA YA UAMUSHO WA ROHO MTAKATIFU
09:02:00
No comments
>>SEMINA>> UAMSHO WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA. NA MWL. ALBERT MWASHAMBWA<<
Uamusho wa roho mtakatifu nini?
contents: 1. Maana ya uamusho wa roho mtakatifu katika kanisa ni nini?
UAMSHO WA ROHO MTAKATIFU; ni hali ya kanisa kuwajibika kulingana na utendaji kazi wa roho mtakatifu au is a state of a church to respond according to holy spirit working. mchanganuo wa maana ya uamsho wa roho mtakatifu.
hali ni mabadiliko ya mtu ambayo yanaweza kutokeza nje na kuleta matokeo. hali ndio inayoweza kufanya mtu aonekane vile anaonekana, lakini pia hali hufanya matokeo ya maamuzi anyofanya mtu na hi huletw na nguvu au msukumo au nguvu inayofanya maamuzi ndani ya mtu.
kama tuluvyokwisha kuona kuwa uamusho wa roho mtakatifu nini. tunaweza kusema kuwa ;
UAMUSHO WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA
2. maana ya uamusho katika maneno "uamusho"
3. Roho mtakatifu ni nani?
4. Roho mtakatifu ni nini juu ya mtu.
5. Roho mtakatifu ndani ya mtu ni nini.
6. Roho mtakatifu kama maji.
7. Roho mtakatifu kama moto.
8. tabia za Roho mtakatifu.
9.Kazi za Roho mtakatifu.
10. Wajibu wa kufanya kuwa na Roho mtakatifu.
Uamusho wa roho mtakatifu nini?
contents: 1. Maana ya uamusho wa roho mtakatifu katika kanisa ni nini?
UAMSHO WA ROHO MTAKATIFU; ni hali ya kanisa kuwajibika kulingana na utendaji kazi wa roho mtakatifu au is a state of a church to respond according to holy spirit working. mchanganuo wa maana ya uamsho wa roho mtakatifu.
hali ni mabadiliko ya mtu ambayo yanaweza kutokeza nje na kuleta matokeo. hali ndio inayoweza kufanya mtu aonekane vile anaonekana, lakini pia hali hufanya matokeo ya maamuzi anyofanya mtu na hi huletw na nguvu au msukumo au nguvu inayofanya maamuzi ndani ya mtu.
kama tuluvyokwisha kuona kuwa uamusho wa roho mtakatifu nini. tunaweza kusema kuwa ;
UAMUSHO WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA
2. maana ya uamusho katika maneno "uamusho"
3. Roho mtakatifu ni nani?
4. Roho mtakatifu ni nini juu ya mtu.
5. Roho mtakatifu ndani ya mtu ni nini.
6. Roho mtakatifu kama maji.
7. Roho mtakatifu kama moto.
8. tabia za Roho mtakatifu.
9.Kazi za Roho mtakatifu.
10. Wajibu wa kufanya kuwa na Roho mtakatifu.
MKUTANO MKUBWA WA INJILI NA CASFETA TAYOMI SJUT
03:48:00
No comments
KARIBUNI WOTE KWENYE MKUTANO MKUBWA WA INJILI NA CASFETA TAyOMI SJUT. KANISA LA FPCT KIKUYU KUANZIA TAR.25-29/01/2017.
mkutano huo unafanyikia katika eneo la kanisa la FPCT KIKUYU. Wahubiri katika mkutano huo ni wanacasfeta wenyewe, ambao miongoni mwao ni EV. IISSACK SUDI na EV. ELIYA SAMWELI na EV. HALINGA FAUSTINE.Wenye shida mbalimbali watafanyiwa maombi na kuponywa kwa jina la YESU KRISTO.
neno la Mungu linasema "Akawaambia enendeni ulimwenguni mwote mukaihubiri injili kwa kila kiumbe. Aaminie na kubatizwa ataokoka asiyeamini atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya.watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha hakita wadhuru kabisa, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya"(marko 16:15-18)
in english
He said to them, “Go into all the world and preach the good news to all creation. Whoever believes and is baptised will be saved, but whoever does not believe will be condemned. And these signs will accompany those who believe: In my name they will drive out demons; they will speak in new tongues; they will pick up snakes with their hands; and when they drink deadly poison, it will not hurt them at all; they will place their hands on sick people, and they will get well.” After the Lord Jesus had spoken to them, he was taken up into heaven and he sat at the right hand of God. Then the disciples went out and preached everywhere, and the Lord worked with them and confirmed his word by the signs that accompanied it.(mark 16:115-20)
USHUHUDIAJI KATIKA WIKI YA USHUHUDIAJI TAR. 06-13/01/2017
03:45:00
No comments
Ushuhudiaji kama agizo ambalo tumepewa na Mungu. ni sehemu moja wapo ambayo CASFETA-TAYOMI SJUT wanamtumikia mungu kwa njia hiyo. tarehe 6 siku ya jumaosi ya kwanza ya mwaka 2017 ushuhudiaji ulianza katika chuo kuku cha ST. JOHN'S UNIVERSITY OF TANZANI.
Ushuhudiaji huo ulifanyika ndani ya chuo katka madarasa na sehemu wanazoishi wanachuo hao. wako waliofunguliwa na kuponywa siku hiyo pia watu kadha wa kadha walimpokea YESU kuwa BWANA na mwokozi wa mwokozi wa maisha yao.
hitimisho katika siku hiyo ilifanyikia eneo la mdegree ambapo EV. FAUSTINE HALINGA alihubiri akishirikiana na EV ISSACK SUDI.>>>MAHUBIRI SIKU YA USHUHUDIAJI MDEGREE KATIKA CHUO KIKUU CHA ST. JOHN'S UNVERSITY OF TANZANIA. NA EV. HALINGA FAUSTINE & EV. ISSACK SUDI.
Ushuhudiaji huo ulifanyika ndani ya chuo katka madarasa na sehemu wanazoishi wanachuo hao. wako waliofunguliwa na kuponywa siku hiyo pia watu kadha wa kadha walimpokea YESU kuwa BWANA na mwokozi wa mwokozi wa maisha yao.
hitimisho katika siku hiyo ilifanyikia eneo la mdegree ambapo EV. FAUSTINE HALINGA alihubiri akishirikiana na EV ISSACK SUDI.>>>MAHUBIRI SIKU YA USHUHUDIAJI MDEGREE KATIKA CHUO KIKUU CHA ST. JOHN'S UNVERSITY OF TANZANIA. NA EV. HALINGA FAUSTINE & EV. ISSACK SUDI.
Wednesday 26 October 2016
KARIBUNI FRESHER'S WOTE CASFETA TAYOMI SJUT
04:02:00
No comments
Uongozi wa CASFETA TAYOMI SJUT unapenda kuwakaribisha wanachuo wote walijiunga na mwaka wa masomo 2016/2017na wengineo kwenye ibada zinazofanyia chuoni ST JOHN.CASFETA TAYOMI inajumuisha wakristo wote wanaotoka makanisa mbalimbali ya kipentekoste nchini Tanzania na hata nje ya nchi mf wa makanisa hayo ni TAG,EAGT,PEFA,WINNERS,PAG,CAG na mengineyo.Hivyo uongozi unapenda kuwakaribisha wanavyuo wote waliojiunga mwaka huu wa masomo kufika katika ibada hizo.
MKARIBISHE NA MWINGINE MUNGU AKUBARIKI
Wednesday 14 September 2016
MKUTANO SIKU YA 3
01:51:00
No comments
Nimuendelezo wa mkutano ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano huu unaoendelea hapa LUBAGA-SHINYANGA,Yesu amekuwa akitenda miujiza na ishara mbalimbali na huku tukishuhudia watu wengi wakimpokea YESU kuwa Bwana na Mwokozi wao,Jumla ya watu 315 waliokoka hii ikiwa ni watu 300 walmpokea Yesu kwa njia ya ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba na watu 15 kwenye mkutano wa jioni.
JUKWAA KABLA YA MKUTANO KUANZA,FUNDI MITAMBO WAKIWEKA MAMBO SAWA |
WANACASFETA WAKIMSIFU MUNGU WAKATI WA MKUTANO |
KWAYA YA LUBAGA WAKIIMBA |
CHOSEN GENERATION BAND WAKIMSIFU MUNGU WAKATI WA MKUTANO |
WANACASFETA WAKIMCHEZEA MUNGU |
NA WATOTO NAO WALIKUWA WAKIMSIFU MUNGU |
WANACASFETA WAKIJIANDAA KUIMBA WAKATI WA MKUTANO |
WAHUDUMU NAO WAKIWA TAYARI KUKUSANYA SADAKA |
MWIMJILISTI NEEMA NGILIULE AKIMHUBIRI YESU |
MWINJILISTI NEEMA NGILIULE AKISISITIZA JAMBO |
WATU WAKIENDA MBELE KUOMBEWA NA KUMPOKEA YESU KRISTO |
WALIOKUWA WAKIMPOKEA YESU KRISTO WAKIOMBEWA BARAKA NA KUFUNGULIWA KATIKA VIFUNGO MBALIMBALI |
WALIOKUWA WAKIMPOKEA YESU KRISTO WAKIOMBEWA BARAKA NA KUFUNGULIWA KATIKA VIFUNGO MBALIMBALI
Tuesday 13 September 2016
MKUTANO MKUBWA WA INJILI SHINYANGA-LUBAGA, NA CASFETA TAYOMI ST JOHN(SJUT)
01:46:00
No comments
Mkutano mkubwa wa injili ulioanza tarehe 10-18/09/2016 maeneo ya lubaga shinyanga,Umekuwa wa tofauti na wenye nguvu za Mungu,yafuatayo ni matukio mbalimbali kuanzia mwanzo wa mkutano na kuendelea hadi mwisho.Ikiwa ni siku ya pili tu ya mkutano jumla ya watu 155 walimpokea YESU hii ikijumuisha mkutano wa mchana,ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba na SINEMA ya usiku
Wana ST JOHN wakiwa ndani ya BASI wakitoka DODOMA kuelekea LUBAGA/SHINYANGA
Mwimbaji kutoka UGANDA Akimsifu MUNGU katika Viwanja vya mkutano IEAGT -LUBAGA SHINYANGA
SIKU YA KWANZA NA YA PILI
Mlezi SULEMANI KURWAkushoto akiwa pamoja na mwenyekiti watawi ISACK SUDI,Mwenyekiti mstaafu Patric JOHN CHUWA na wahubiri wengine ,dada NEEMA NGILIULE na Mwinjilisti ELIYA
Mwimbaji kutoka UGANDA Akimsifu MUNGU katika Viwanja vya mkutano IEAGT -LUBAGA SHINYANGA
Wahudhuriaji wa Mkutano wakifuatilia mkutano kwa Makini
JC CHOIR wakimsifu Mungu
IEAGT CHOIR wakimsifu MUNGU katika mkutano
DADA CLENE DOTTO akiendelea na Maombi wakati mkutano ukiendelea |
KWAYA ya CASFETA ST JOHN wakijiandaa kumuimbia MUNGU katiaka mkuano huo
Wahudumu wamkutano wakiwa mbele ya jukwaa tayari kwa kufanya huduma
Praise Team wakimwabudu Mungu
MHUBIRI WA MKUTANO mwinjilist ISACK SUDI akiwa tayari kumhubiri YESU KRISTO
Wana SJUT wakiwa na matawi na vuvuzela kwa ajili ya kumshangilia Mungu wakati wa Mahaubiri
WATU wakiwa mbele kwa ajili ya kuombewa
Waongofu waya wakiwa mbele ya mkutano tayari kwa kumpokea YESU KRISTO
Subscribe to:
Posts (Atom)