UCHUMI NA MKRISTO
SI
MAPENZI YA MUNGU TUWE NA MAISHA DUNI/ MASKINI
Napenda kuanza
kukuambia ya kuwa si mapenzi ya Mungu uwe maskini. Kwa sababu tangu kuwekwa
misingi ya ulimwengu huu, Mungu hakupanga kuwa watu wake aliowaumba wawe
maskini; bila kujali rangi, kabila, wala taifa. ( Kumbuka EFESO 3:20;)
Mtu
maskini maana yake ni mtu mhitaji. Mtu aliye maskini wa
mambo ya mwili ni yule aliye mhitaji wa mambo ya mwili. Na mambo ya mwilini
ninayoyasema ni mavazi, chakula na mahali pa kulala. Yesu Kristo hakusema heri
wale walio na mahitaji ya chakula, mavazi, afya na malazi.
Japo ni
imeandikwa katika Mithali 22:2, kuwa “Tajiri na maskini hukutana pamoja;
Bwana ndiye aliyewaumba wote”. Lakini fahamu ya kuwa ingawa matajiri na maskini
waliopo wote waliumbwa na Mungu; tangu mwanzo wa uumbaji Mungu hakuyaweka
matabaka haya mawili.
SABABU 4 KWA
NINI SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASIKINI.
- Mungu
ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri
“ Bali utamkumbuka Bwana , Mungu wako,
maana ndiye akupaye NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; ili alifanye
imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo” (Kumb. 8:18).
Lakini fahamu ya kuwa si matajiri wote waliopo duniani
wameupata utajiri kutokana na nguvu walizopewa na Mungu. Wengi wamepata utajiri
kwa njia ya dhuluma. Na ndiyo maana sehemu nyingi katika Biblia matajiri wa
jinsi hiyo wamekemewa. Soma Amosi 5:11, 12. Kwa sababu hii Mungu hayuko upande
wa matajiri hawa. Hii pia haimaanishi kuwa Mungu yuko upande wa KILA
maskini aliopo duniani. La hasha! Mungu yuko upande wa yule ayafanyaye mapenzi
yake awe tajiri au maskini (Mathayo 7:21)
- Mungu
ndiye atufundishaye kupata faida
Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo
Yesu si Mungu wa hasara bali Mungu wa faida. Imeandikwa hivi; “ Bwana, Mkombozi wako, Mtakatifu wa
Israeli, asema hivi;Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye
ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuifuata” (Isaya
48:17).
- Vitu
vyote vyema ni mali ya Bwana, na vyote vya Bwana ni vyetu ndani ya Kristo
Katika Zaburi 24:1 imeandikwa;“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya
Bwana; Dunia na wote wakaao ndani yake”
Na pia ukisoma katika Hagai 2:8 unaona imeandikwa hivi “Fedha ni mali yangu, na
dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi”
- Yesu
Kristo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri
“ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi
alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi
mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” (2 Wakorintho 8:9).
Je! unafahamu kwa nini
Yesu Kristo aliamua kuwa maskini? Ni “…….. ili kwamba ninyi mpate kuwa MATAJIRI
kwa umaskini wake”.
Najua kuna wengine watashangaa
kuusoma mstari huu; lakini ndivyo ilivyo. YESU ansema Na ndiyo maana alisema
katika Luka 4:18a ya kuwa; “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia
mafuta kuwahubiri MASKINI habari njema.”
Mtume Petro naye aliwahi kusumbuliwa sana na jambo
hili, hata ikabidi amuulize Bwana Yesu.
“Ndipo
Petro akajibu, akamwambia, tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata, TUTAPATA
NINI BASI?” (Mathayo 19:27)
“Yesu akasema, Amini, nawaambiaeni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu
waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili
yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa MARA MIA SASA WAKATI HUU, nyumba, na
ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia;
na katika ulimwengu ujao uzima wa milele” (Marko 10:29,30).
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa
maarifa ……." (Hosea 4:6). Maneno haya yaliyosemwa na
Mungu kwa kinywa cha Nabii Hosea yana ukweli ndani yake hata hivi leo. Watu
wengi sana siku hizi wanaangamizwa, wanadhulumiwa, wanahuzunishwa na maisha kwa
sababu tu wamekosa kuyajua maarifa ya Mungu yaliyomo katika Neno lake.
Tulikuwa tunafurahi tunaposoma mstari kama ufuatao; "
…..vyote ni vyenu …. Vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni
vyenu, nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu" (Wakorintho
3:21,22). Tulikuwa tunafurahi kwa kuwa maneno haya yanatupa uhalali wa kumiliki
vitu vilivyo vya Mungu. Kwa mfano Hagai 2:8 inasema "Fedha ni mali
yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa Majeshi." Pia, Zaburi
24:1 inasema "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana …"
Lakini jambo lililotusumbua ni kwamba ingawa mistari hiyo ilitupa umilikaji juu
ya fedha, dhahabu na vyote viijazavyo nchi ili tuvitumie – SISI HATUKUWA NAVYO
WALA HATUKUJUA TUTAVIPATAJE!
Tulitamani sana kuona maneno ya Wafilipi 4:19
yanatimia kwetu – nayo yanasema hivi;
"Na Mungu wangu atawajazeni kila
mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo
Yesu".
·
Lakini mnaweza kushinda kwa kusimama katika Neno langu ambalo ni upanga wa Roho
mikononi mwenu.
·
Nimesema katika Yoshua 1:8 ya kuwa mtafanikiwa ikiwa mambo matatu yatafanyika
juu ya Neno langu:
(a) Lisiondoke kinywani mwenu
(b) Mlitafakari wakati wote
(c) Na kudumu kulitenda
Ahsante,
KANUNI
ZA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA KWA
MWAMINI/MKRISTO:
usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako na
kuukuza uzalishaji wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini
kama una usimamzi mbaya wa fedha uchumi wako utayumba tu.Matatizo mengi
ya kifedha tunakimbilia kuombewa na kukemea,lakini hayo yote bila
kujifunza usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika mzizi.hata
ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha matatizo ya kifedha yatarudi baada ya muda
mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi kanuni za fedha.
1: JIFUNZE
KUWEKA NA KUWEKEZA AKIBA USILE
KILA KITU UPATAPO TOKA KWA BWANA!
Kosa
Kubwa Wanalofanya Wana Wa Mungu, Hasa Wale Waliookoka, Wanaoishi Kwa Imani, Ni
Kutojua Kuwa Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Ndani Ya Muda Maalumu, Na Hurudi
Kutupa Tena Baada Ya Muda, Na Sio Kwamba Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Kila
Siku… Hii Naizungumzia Kwenye Maeneo Ya Mahitaji Yetu Ya Kifedha, Chakula,
Vyakula, Mavazi Nk… Mungu Anapokupa Kitu, Mahitaji Yako, Huwa Anakupa NA ZIADA,
Hakupi Kipimo Cha Kula Au Kutumia Muda Ule Tu… Huwa Anatoa NA CHA ZIADA AU
NYONGEZA JUU… Lengo Kubwa La Mungu Kukupa KITU CHA ZAIDI AU ZIADA Ni Ili
Akusaidie Kwenye KESHO YAKO (Future)… Narudia Tena, Mungu Huwa Anatupa Na
Ziada, Lengo Lake Kubwa Ni Kufidia MUDA ULIOPO KATIKATI HAPA Kati Ya Pale
Alipokupa Hadi Pale Atakaporudi Tena Kukupatia Tena! MWANZO 41:25-35,48,49.
NDIO MAANA Mungu Anatufundisha Habari Za Chungu, Wasio
Na Msimamizi Wala Kiongozi Ambao Wakati Wa MAVUNO Hawali Chakula Chote Bali
HUJIWEKEA AKIBA Inayowasaidia Wakati Wa UKAME NA NJAA MITHALI 6:6-8 NA 30:24-25…
Lakini Pia Mara Nyingi Kwenye NENO LAKE, Mungu
Amezungumza Kuhusu GHALA… Ambayo Ni Sehemu Ya Kuhifadhia Au Kutunzia MAVUNO/
ULICHOPATA Kwa Ajili Ya KESHO YAKO… Pia Mungu Mara Nyingi Amesema Kuhusu
HAZINA… Inayomaanisha SHEHENA ILIYOHIFADHIWA Kwa Ajili Ya MATUMIZI YA BAADAYE…
Na Mara Nyingi Mungu Anapokuja KUTUBARIKI, Huwa Analenga HAZINA NA GHALA ZETU…
Utamsikia Akisema, “Nipate KUZIJAZA HAZINA NA GHALA ZENU” (Malaki 3:10).
Lakini Hata Yesu Mwenyewe Alijua Kanuni Hii Na Aliitendea Kazi… Hata Wakati
Alipowalisha Wale Wanaume 5000, Wanawake Wengi Na Watoto, BADO YEYE NA TIMU
YAKE WALIKUSANYA CHAKULA KILICHOBAKI
(Marko 6:42-43, Yohana 6:12-13)
YESU Alikuwa Na Uelewa Wa Kutosha Kuhusu
Mungu, Baba Yake Ya Kuwa Huwa Anatoa ZIADA, Lakini Usipoitunza Na KUTUMIA KILA
ULICHOPATA, BILA KUWEKA AKIBA, Kuna Muda Unakuja Ambao Utakuwa Na Uhitaji Na
Hata Ukimlilia Na Kumwita Mungu, HATAKUJIBU AU KUKUPA Kingine Mpaka Muda Ule
Aliopanga Utakapofika!
Mungu Anapokufungulia MLANGO Wa Kupata MSHAHARA, Au
Kipato Kizuri Kwenye Biashara Au Shughuli Zako Za Uzalishaji, USITUMIE KILA
ULICHOPATA… JIWEKEE AKIBA… WEKA GHALANI Kwa Ajili Ya Kesho Yako Au Itumie Ile
Ziada Kwa Ajili Ya KUZALISHA FAIDA ZAIDI [WEKEZA ILE ZIADA] Kwenye shughuli Au
Jambo Litakalokupa Zaidi Ya Ile Na Kukuvusha Kipindi Cha UGUMU Kitakapokuja!
Jifunze Kuweka Akiba… Lakini Mara Baada Ya Kupata Hiyo Akiba, Iwekeze Mahali
Ambapo Unaweza Kuiongeza Ili Uwe SALAMA Wakati Wenzako Watakopokuwa WANALIA
NJAA
2.
TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA NA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA
Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza kukusaidia
katika kuandaa bajeti yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari ndogo na anza
kuweka kumbukumbu za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini itakusaidi
kwa mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa
usafiri?simu?chakula?matibabu?chakula n.k ni lazima ujue wapi fedha yako
inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina mililki nini, nina nini,
nina daiwa,natuamiaje (MITHALI 27:23-24,
23:23,)
3.
JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU, KWA NANI NA KWA UTARATIBU.
(Mithali 11:24-25).kanuni ya uchumi wa Kimungu ni
tofauti,kadiri unavyotoa na sivyo unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako
unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa kwaajili ya kuwabariki wengine,kutoa kwaajili ya
wahitaji(Mithali 28:27 Mithali 11:25.Mithali 19:17,Mithali 3:9-10),Kutoa
kunafungua Baraka za Mungu katika Maisha yako.
(A) tumia fedha yako
kwa hekima na ridhika na ulicho nacho:
Zingatia vipaumbele
na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila mpangilio,manunuzi ya papo kwa
papo,usifanye matumizi yaliyo nje,yanayozidi kipato chako au uwezo wako wa
kifedha.Jifunze kuridhika na kuuepuka tamaa.usifuje fedha kwa matumizi ya
ovyo.jifunze kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9)
Alex John Wambi,
Mwalim,FPCT Chamwino.
0 comments:
Post a Comment