1. MAANA YA KUOKOKA
Kuokoka ni kitendo cha kuzaliwa m
ara ya pili yaani kuzaliwa kwa roho.
YOHANA 1:12-13 “ bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Ndio wale waliaminio jina lake(YESU). Wamezaliwa si kwa damu(ukoo), si kwa mapenzi ya mwili wala kwa mapenzi ya mtu(vikao) bali kwa mapenzi ya Mungu.
Wokovu ni neema na mapenzi ya Mungu tu na si vinginevyo, si kwa ajili ya kumfurahisha aliye kushuhudia neno, mhubiri, mzazi, dhehebu, dini au kabila Fulani.
WAEFESO 2 : 8, 9 “kwa maana mmeokolewa kwa neeema kwa njia ya imani ambayo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa(uwezoau nguvu ) cha Mungu. Msitari wa tisa(9) “ si kwa matendo (wema au uzuri au elimu au mali au kimo chako ) mtu awaye yote asije akajisifu” yaani asiwe na kiburi kwa sababu AMEOKOKA.
Kuokoka ni kupata sifa ya kuingia katika ufalme wa Mungu. YOHANA 3: 5-6 “mtu asipozaliwa kwa maji(ubatizo wa maji mengi) na kwa ROHO(IMANI) hawezi kuingia katika ufalme w Mungu.
KUOKOKA ni kufanywa upya baada ya kuuvua utu wa kale au mwenendo( tabia) WAEFESO 4:22-24 ‘vueni kwa habari ya mwenndo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kuzifuata tama zidanganyazo mfanywe upya, mkavae utu upya ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
2. HATUA MBILI ZA KUCHUKUA WAKATI WA KUOKOKA
WARUMI 10: 9-10
(i) KUKIRI;- Ukimkiri(kutamka) kwa kinywa chako yakuwa YESU kristo ni BWANA na mwokozi wa maisha yako UTAOKOKA.
(ii) KUAMINI;- Ukiamini kuwa MUNGU alimleta yesu duniani akazaliwa, akafa kwa ajili ya dhambi zako na akafufuka kutoka katika wafu UTAOKOKA.
3. KWA NINI TUNAOKOLEWA KWA NJIA YA IMANI?
(I) Kwa sababu lazima ubadili imani yako iliyojengwa katika mizimu, uganga, upagani, uchawi, uisramu, matambiko, kafara n.k. sas umwamini MUNGU wa miungu na Bwana wa mabwana ambaye imani ktika yeye imejengw katika neno lake . WARUMI 10:17- “basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo(YESU)
(II) Kwa sababu pasipo imani haiwezekani kumpendeza MUNGU,
WAEBRANIA 11:6 –“ pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila amwendeaye(anyetaka kuwa mtoto MUNGU) lazima aamini ya kwamba MUNGU yupo na kwamba huwapa thawabu(Baraka, kibali, majibu) wale wamtafutao”
4. MAMBO MHIMU YA KKUZINGATIA BAADA YA KUOKOKA.
(a) Wokovu unapatikana kwa YESU pekee, si katika dini au mtume au nabii au dhehebu lolote. Usianganyike.
MATENDO 4:12. Toba ndio njia pekee yakumrud ia na kutengeneza na MUNGU na kutafuta amani. MATENDO 3:19, 1YOHANA 1:8-9( kwa toba tunapata ondoleo la dhambi)
(b) Epuka tama zipinganazo na roho na jitahidi kutenda mema. 1PETRO 2 : 11-12, zingatia sana YAKOBO 4: 17 biblia inasema “ yeye ajuaye kutanda mema na wala hayatendi kwake huyo ni dhambi”.
(c) Mtii MUNGU daima na mpinge shetani mara zote yeye pamoja na ushawishi wake wote. YAKOBO 4:7 “ basi mtiini MUNGU mpingeni shetani, mkalibieni MUNGU nae atawakaribia ninyi.
(d) Kaa ndani ya YESU ili upate kuzaa sana, kustawi, kufanikiwa. YOHANA 15:1-17.
(e) Tafuta kanisa la watu waliookoka ili ukamwabudu MUNGU huko, ili ukue kuroho. MATENDO 2:4-42
ishi kwa kumaanisha maisha ya wokovu(kubali kubadilika, kubali kubatizwa na kujifunza neno ili uwe mwanafunzi wa yesu. MATHAYO 28:19-20.
SALA YA TOBA
“BWANA YESU nakiri mimi ni mwenye dhambi, naomba unisamehe dhambi zote nilizozitenda kwanza kwa maneno na kwa matendo unitakase kwa damu yako, karibu moyoni mwangu, uwe BWANA NA MWOKOZI wa maisha yangu, naomba ufute jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima, wewe shetani kuanzia leo! Ninakukataa na kazi zako zote, BWANA YESU naomba ROHO mtakatfu anisaidie kuishi maisha matakatifu, kwa jina la YESU Kristo naamini NIMEOKOKA AMENI!
posted by MR. BOAZ ELIYA,
edited by evanglism departiment
cooperating with EV. DASTAN
posted by MR. BOAZ ELIYA,
edited by evanglism departiment
cooperating with EV. DASTAN
UCHUMI NA MKRISTO by ALEX JOHN WAMBI. MWALIMU WA FPCT CHAMWINO DODOMA.
UCHUMI NA MKRISTO
SI MAPENZI YA MUNGU TUWE NA MAISHA DUNI/ MASKINI
Napenda kuanza kukuambia ya kuwa si mapenzi ya Mungu uwe maskini. Kwa sababu tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu huu, Mungu hakupanga kuwa watu wake aliowaumba wawe maskini; bila kujali rangi, kabila, wala taifa. ( Kumbuka EFESO 3:20;)
Mtu maskini maana yake ni mtu mhitaji. Mtu aliye maskini wa mambo ya mwili ni yule aliye mhitaji wa mambo ya mwili. Na mambo ya mwilini ninayoyasema ni mavazi, chakula na mahali pa kulala. Yesu Kristo hakusema heri wale walio na mahitaji ya chakula, mavazi, afya na malazi.
Japo ni imeandikwa katika Mithali 22:2, kuwa “Tajiri na maskini hukutana pamoja; Bwana ndiye aliyewaumba wote”. Lakini fahamu ya kuwa ingawa matajiri na maskini waliopo wote waliumbwa na Mungu; tangu mwanzo wa uumbaji Mungu hakuyaweka matabaka haya mawili.
SABABU 4 KWA NINI SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASIKINI.
- Mungu ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri
“ Bali utamkumbuka Bwana , Mungu wako, maana ndiye akupaye NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo” (Kumb. 8:18).
Lakini fahamu ya kuwa si matajiri wote waliopo duniani wameupata utajiri kutokana na nguvu walizopewa na Mungu. Wengi wamepata utajiri kwa njia ya dhuluma. Na ndiyo maana sehemu nyingi katika Biblia matajiri wa jinsi hiyo wamekemewa. Soma Amosi 5:11, 12. Kwa sababu hii Mungu hayuko upande wa matajiri hawa. Hii pia haimaanishi kuwa Mungu yuko upande wa KILA maskini aliopo duniani. La hasha! Mungu yuko upande wa yule ayafanyaye mapenzi yake awe tajiri au maskini (Mathayo 7:21)
- Mungu ndiye atufundishaye kupata faida
Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo Yesu si Mungu wa hasara bali Mungu wa faida. Imeandikwa hivi; “ Bwana, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi;Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuifuata” (Isaya 48:17).
- Vitu vyote vyema ni mali ya Bwana, na vyote vya Bwana ni vyetu ndani ya Kristo
Katika Zaburi 24:1 imeandikwa;“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana; Dunia na wote wakaao ndani yake”
Na pia ukisoma katika Hagai 2:8 unaona imeandikwa hivi “Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi”
- Yesu Kristo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri
“ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” (2 Wakorintho 8:9).
Je! unafahamu kwa nini Yesu Kristo aliamua kuwa maskini? Ni “…….. ili kwamba ninyi mpate kuwa MATAJIRI kwa umaskini wake”.
Najua kuna wengine watashangaa kuusoma mstari huu; lakini ndivyo ilivyo. YESU ansema Na ndiyo maana alisema katika Luka 4:18a ya kuwa; “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri MASKINI habari njema.”
Mtume Petro naye aliwahi kusumbuliwa sana na jambo hili, hata ikabidi amuulize Bwana Yesu.
“Ndipo Petro akajibu, akamwambia, tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata, TUTAPATA NINI BASI?” (Mathayo 19:27)
“Yesu akasema, Amini, nawaambiaeni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa MARA MIA SASA WAKATI HUU, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele” (Marko 10:29,30).
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ……." (Hosea 4:6). Maneno haya yaliyosemwa na Mungu kwa kinywa cha Nabii Hosea yana ukweli ndani yake hata hivi leo. Watu wengi sana siku hizi wanaangamizwa, wanadhulumiwa, wanahuzunishwa na maisha kwa sababu tu wamekosa kuyajua maarifa ya Mungu yaliyomo katika Neno lake.
Tulikuwa tunafurahi tunaposoma mstari kama ufuatao; " …..vyote ni vyenu …. Vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu, nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu" (Wakorintho 3:21,22). Tulikuwa tunafurahi kwa kuwa maneno haya yanatupa uhalali wa kumiliki vitu vilivyo vya Mungu. Kwa mfano Hagai 2:8 inasema "Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa Majeshi." Pia, Zaburi 24:1 inasema "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana …" Lakini jambo lililotusumbua ni kwamba ingawa mistari hiyo ilitupa umilikaji juu ya fedha, dhahabu na vyote viijazavyo nchi ili tuvitumie – SISI HATUKUWA NAVYO WALA HATUKUJUA TUTAVIPATAJE!
Tulitamani sana kuona maneno ya Wafilipi 4:19 yanatimia kwetu – nayo yanasema hivi;
"Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu".
· Lakini mnaweza kushinda kwa kusimama katika Neno langu ambalo ni upanga wa Roho mikononi mwenu.
· Nimesema katika Yoshua 1:8 ya kuwa mtafanikiwa ikiwa mambo matatu yatafanyika juu ya Neno langu:
(a) Lisiondoke kinywani mwenu
(b) Mlitafakari wakati wote
(c) Na kudumu kulitenda
Ahsante,
KANUNI ZA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA KWA MWAMINI/MKRISTO:
usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako na kuukuza uzalishaji wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini kama una usimamzi mbaya wa fedha uchumi wako utayumba tu.Matatizo mengi ya kifedha tunakimbilia kuombewa na kukemea,lakini hayo yote bila kujifunza usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika mzizi.hata ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha matatizo ya kifedha yatarudi baada ya muda mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi kanuni za fedha.
1: JIFUNZE KUWEKA NA KUWEKEZA AKIBA USILE KILA KITU UPATAPO TOKA KWA BWANA!
Kosa Kubwa Wanalofanya Wana Wa Mungu, Hasa Wale Waliookoka, Wanaoishi Kwa Imani, Ni Kutojua Kuwa Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Ndani Ya Muda Maalumu, Na Hurudi Kutupa Tena Baada Ya Muda, Na Sio Kwamba Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Kila Siku… Hii Naizungumzia Kwenye Maeneo Ya Mahitaji Yetu Ya Kifedha, Chakula, Vyakula, Mavazi Nk… Mungu Anapokupa Kitu, Mahitaji Yako, Huwa Anakupa NA ZIADA, Hakupi Kipimo Cha Kula Au Kutumia Muda Ule Tu… Huwa Anatoa NA CHA ZIADA AU NYONGEZA JUU… Lengo Kubwa La Mungu Kukupa KITU CHA ZAIDI AU ZIADA Ni Ili Akusaidie Kwenye KESHO YAKO (Future)… Narudia Tena, Mungu Huwa Anatupa Na Ziada, Lengo Lake Kubwa Ni Kufidia MUDA ULIOPO KATIKATI HAPA Kati Ya Pale Alipokupa Hadi Pale Atakaporudi Tena Kukupatia Tena! MWANZO 41:25-35,48,49.
NDIO MAANA Mungu Anatufundisha Habari Za Chungu, Wasio Na Msimamizi Wala Kiongozi Ambao Wakati Wa MAVUNO Hawali Chakula Chote Bali HUJIWEKEA AKIBA Inayowasaidia Wakati Wa UKAME NA NJAA MITHALI 6:6-8 NA 30:24-25…
Lakini Pia Mara Nyingi Kwenye NENO LAKE, Mungu Amezungumza Kuhusu GHALA… Ambayo Ni Sehemu Ya Kuhifadhia Au Kutunzia MAVUNO/ ULICHOPATA Kwa Ajili Ya KESHO YAKO… Pia Mungu Mara Nyingi Amesema Kuhusu HAZINA… Inayomaanisha SHEHENA ILIYOHIFADHIWA Kwa Ajili Ya MATUMIZI YA BAADAYE… Na Mara Nyingi Mungu Anapokuja KUTUBARIKI, Huwa Analenga HAZINA NA GHALA ZETU… Utamsikia Akisema, “Nipate KUZIJAZA HAZINA NA GHALA ZENU” (Malaki 3:10).
Lakini Hata Yesu Mwenyewe Alijua Kanuni Hii Na Aliitendea Kazi… Hata Wakati Alipowalisha Wale Wanaume 5000, Wanawake Wengi Na Watoto, BADO YEYE NA TIMU YAKE WALIKUSANYA CHAKULA KILICHOBAKI
(Marko 6:42-43, Yohana 6:12-13)
YESU Alikuwa Na Uelewa Wa Kutosha Kuhusu Mungu, Baba Yake Ya Kuwa Huwa Anatoa ZIADA, Lakini Usipoitunza Na KUTUMIA KILA ULICHOPATA, BILA KUWEKA AKIBA, Kuna Muda Unakuja Ambao Utakuwa Na Uhitaji Na Hata Ukimlilia Na Kumwita Mungu, HATAKUJIBU AU KUKUPA Kingine Mpaka Muda Ule Aliopanga Utakapofika!
Mungu Anapokufungulia MLANGO Wa Kupata MSHAHARA, Au Kipato Kizuri Kwenye Biashara Au Shughuli Zako Za Uzalishaji, USITUMIE KILA ULICHOPATA… JIWEKEE AKIBA… WEKA GHALANI Kwa Ajili Ya Kesho Yako Au Itumie Ile Ziada Kwa Ajili Ya KUZALISHA FAIDA ZAIDI [WEKEZA ILE ZIADA] Kwenye shughuli Au Jambo Litakalokupa Zaidi Ya Ile Na Kukuvusha Kipindi Cha UGUMU Kitakapokuja!
Jifunze Kuweka Akiba… Lakini Mara Baada Ya Kupata Hiyo Akiba, Iwekeze Mahali Ambapo Unaweza Kuiongeza Ili Uwe SALAMA Wakati Wenzako Watakopokuwa WANALIA NJAA
2. TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA NA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA
Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza kukusaidia katika kuandaa bajeti yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari ndogo na anza kuweka kumbukumbu za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini itakusaidi kwa mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa usafiri?simu?chakula?matibabu?chakula n.k ni lazima ujue wapi fedha yako inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina mililki nini, nina nini, nina daiwa,natuamiaje (MITHALI 27:23-24, 23:23,)
3. JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU, KWA NANI NA KWA UTARATIBU.
(Mithali 11:24-25).kanuni ya uchumi wa Kimungu ni tofauti,kadiri unavyotoa na sivyo unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa kwaajili ya kuwabariki wengine,kutoa kwaajili ya wahitaji(Mithali 28:27 Mithali 11:25.Mithali 19:17,Mithali 3:9-10),Kutoa kunafungua Baraka za Mungu katika Maisha yako.
(A) tumia fedha yako kwa hekima na ridhika na ulicho nacho:
Zingatia vipaumbele na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila mpangilio,manunuzi ya papo kwa papo,usifanye matumizi yaliyo nje,yanayozidi kipato chako au uwezo wako wa kifedha.Jifunze kuridhika na kuuepuka tamaa.usifuje fedha kwa matumizi ya ovyo.jifunze kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9)
Alex John Wambi,
Mwalim,FPCT Chamwino.
The power of learning: BY Patrick Chuwa
Definition:
Learning is the process of acquiring knowledge, behavior, skills and attitude
as the result of interacting with the environment. The following are some
quotations about learning.
Learning
is a natural pleasure not confined to philosophers only but common to all men.
[Aristotle].
The Bible says that:-
- “A Wiseman will hear and will increase learning and a man of understanding shall attain unto wise counsels”. (Prov 1:5).
- Anyone who stops learning is old whether at age 20/80. Anyone who keeps learning stays young. The greatest thing in life is to keep your mind young (Henry Ford).
- Learn as though you would never be able to master it, hold it as though you would be in a fear of losing it (Confucius).
- If we commit ourselves to reading, thus increasing our knowledge, only God limits how far we can go in this world. (Ben Carson).
- Live as if you were to die tomorrow, learn as if you were to live forever (Mahatma Gandhi).
- All I have learned, I learned them from Books (Abraham Lincoln).
Note:
Books are best source for acquiring knowledge.
Reading has the following
importance
- Reading activates and exercises the mind.
- Reading forces the mind to discriminate. From the beginning, readers have to recognize letters (alphabets) printed on the pages; make them into words, the words into sentences and the sentences into concepts (B. Carson).
- Reading pushes us to use our imagination and makes us more creatively inclined.
- It is chiefly through books that we enjoy intercourse with superior minds. In the best books great men talk to us, give their most precious thoughts, and pour their souls into ours. God be thanked for books. They are the voices for the distant and the dead, and make us heirs of spiritual life of the past ages.Books are true levers. They give to all, who will faithfully use them, the society, the spiritual presence of the best and greatest of our race. (William Ellery Channing).
- If we make every attempt to increase our knowledge in order to use it for human good, it will make a difference in us and in our world (B. Carson).
Note:
If you don’t understand English language take dictionary and read one word
after another, those books are written by normal people like you not angels,
how do you say you don’t understand somebody idea . Think!
Everyone
who knows how to read has it in his power to magnify himself, to multiply the
ways, in which he exists, to make his life full, significant, and interesting.
(Ben Carson). Without knowledge, life is no more than shadow of death
(Moliere). Nothing is so powerful than knowledge and understanding, Francis
Bacon says that “Knowledge is power”. Helen Hayes says that “when books are
opened we discover that we have wings”. The Bible says that “Till I come, give
attendance to reading, to exhortation, to doctrine. 1Thim 4:13” also Paul the
apostle says that “The cloke that I left at Troas with Carpus, when you come
bring with you and BOOKS, but
especially the parchment”. 2Thim 4:13, Paul was a man of depth learning that’s
why he had more revelation than all other apostles.
Dr.
David O. Oyedepo says that “Readers are leaders” The more you read, the more
you lead. Education brings knowledge, knowledge brings power and power brings
respect and respect brings Happiness. Learning gives creativity, creativity
leads to thinking, thinking provides knowledge, knowledge makes you great
(Abdul Kalam).
A
Wiseman once said that “You will be the same person you are in five years times
except for two things: The books you read and the company you keep” .John Dewey
on his philosophical contribution on education says that “education has no end.
It starts from point of birth to death. It is not preparation for life but
rather life itself. Education should aim higher than mere academic or
vocational learning”.
On
the other hand Aggrey’s idea for the aim of education is that: “Education
should be for the development, restitution and self-actualization of society to
levels of knowledge, self-sufficiency, productive abilities, respectability and
equality of consideration among all other segments of humanity.
A
man of God by name T. L. Osborn says that “When you stop learning, you start
dying”
Note:
The best gift which God has given all of us is the MIND.
- A Wiseman says that “The mind is not a vessel to be filled but a fire to be ignited.
- Reading of all books is like conversation with the finest men of past centuries (Descartes). B.B. King says that “the beautiful thing about learning is that no one can take it from you”.
- The man of little learning grows old like the ox, “his body grows but wisdom grows not” (Gautama Buddha).
- Remember a saying that “An empty mind is devils workshop”.
Note:
There is no value in degree; your degree is a personal cup of tea. The value of
your degree is in what you deliver. What are you adding to the society is what
makes your degree valuable. Don’t mistaken schooling for education, for they
are not the same. That’s why today there are so many certificated uneducated
people because they mistaken schooling for education. (Patrick Chuwa).
The difference between
schooling and Education.
- Schooling empowers you for education, schooling is periodic BUT education is for life time.
- Schooling gives you foundation for education.
- Schooling enables us to be literate and then we use our literacy to educate ourselves.
- Education is on – going learning.
- Education is a lifelong learning.
- Schooling facilitates learning and leaning facilitate education.
- Education is the movement from darkness to light (Allan Bloom, philosopher).
The
principle of goal of education in school should be creating men and women who
are capable of doing new things, not simply repeating what other generation
have done (Jean Piaget).
- Education is a continuous building of skills and knowledge throughout the life of an individual.
- Education is freedom (Paulo Freire Philosopher& Brazilian educator).
- Mwalimu Nyerere says that “Living is learning and learning is about trying to live better”.
I
like the speech which was given by our vice chancellor of SJUT Prof. Emmanuel
D. Mbena on Wednesday 10th Feb, 2016 at MH.
He
says “Pursue University education; University
education is university of a certain kind. There is of course the curriculum
and implementation of that curriculum. There are expectations of knowledge,
skills and competences that are intended in that curriculum and its
implementation. Bachelor level is about knowledge acquisition. Masters level is
about knowledge generation. The qualification which you receive at the end of
your study must be a true reflection of your knowledge, skills and competences
for that particular qualification. The minimum requirements are taken to be
sufficient for your attainment of the qualification appertaining to that
qualification.
Prof.
Mbena continues by saying that be sure
to pursue to university education. Do not settle for a level of knowledge
or competence that you did not have to go through university to acquire it. The
mining industry. Be sure to get gold from the goldmine. In your pursuit of such
an education, aim high. Determine to excel in your studies. Don’t say, “You do
not want to fail”, say “you want to excel”, Grow your study skills, work hard,
seek to be extraordinary. But also, in your pursuit of such education, aim far.
Beyond the current qualification, beyond the next qualification. Refuse
mediocrity. Refuse substandard. Shum lack of academic integrity”.
Therefore
never let formal education get in the way of your learning (Mark Twain), “If
you were graduated yesterday and have learned nothing today, you will be
uneducated tomorrow”. “Intellectual growth should commerce at birth and cease
only at death” (Albert Einstein). Education of a man is never completed until
he dies, (Robert E. Lee). Make your brain work. It will sweat, but it will
improve (E. W. Kenyon). Dr .David O. Oyedepo says that “You are either building
a library or a mortuary without knowing”. Abraham Lincoln says that “All I have
learned, I learn them from books” Books are boosters. The Bible says that “I
Daniel understand by books (Daniel 9:2)”.
There
are two people whom I admire in my life. One of them is
Michael Faraday
Michael
Faraday was Physicist and Chemistry in the 19th century. He was
famous British man. He had only two years formal education. He came from poor
family. But Michael Faraday was a lover of knowledge. He educated himself
through private study. He was a book binder.
Michael
Faraday could save money to attend scientific experiments wherever they could
be. One day he bonded a book of 300
pages which contained the lecture notes of Humphrey Davy the professor whom he
attended his seminars and sent to him just to thank him. One day the lab
attendant of Humphrey Davy left and the professor whom he attended his lecture Humprey
Davy remembered that there was one man who sent to him his lectures, and asked
Michael Faraday would you like to become my lab attendant? Michael Faraday
replied yes I would like to be. As he was lab attendant he was busy learning
different scientific experiments. He was involved in the study of Chlorine.
Through
private study:-
- He conducted experiments on diffusion of gases
- He built the first electric motor
- He discovered the so called mutual induction
- He discovered the laws of electrolysis
- He discovered the laws of electromagnetic induction
- He invented the most primitive form of Bunsen burner. Even in the days of Humphrey Davy the professor people said that Michael Faraday was more logical thinker than the Professor.
Note:
Michael Faraday was a lover of God. He was a believer. Wherever he went to
lecture he could ask where can I get church? When he was reading besides him
you will find a Bible. He was an elder in the Presbyterian Church.
- One day they asked him, what do you say about speculations (Life after death), he said: “I am resting on certainties. I know that my redeemer lives and because he lives I shall live also”.
- When Michael Faraday died, he was buried near Isaac Newton tomb to honor him.This is what power of learning is; no matter what family you are coming from if you commit yourself to private studying you will change your world. Your colour is no barrier. Remember God is no respecter of persons: But in every nation including your country he that fears him, and works uprightly before him, he is equally accepted by him. (Acts 10:34-35).
Another
one is whom I admire is
Benjamin Franklin
Benjamin
Franklin was one of the leading figures of early American history. Benjamin
Franklin had little formal education. He had only two years formal education,
but he was a lover of knowledge. He was entirely self – taught. He could spend
his money for food to buy books.
By
age 12 he was serving as indentured apprentice book binder at a printing shop
owned by his brother James. He was reading essays and articles and then writes
them from memory. He educated himself through private study until he became.
- Statesman.
- Author, publisher.
- A great scientist.
- An inventor; he invented lightning conductor.
- He founded a school which later turned to PennsylvaniaUniversity.
- He founded National new paper.
- He invented bifocal glasses, heating stores.
- He built a heart hospital.
- He became philosopher who became a celebrity on both sides of the Atlantic.Franklin unveiled his scheme for new Alphabet and a reformed model of spelling consonants C, J, Q, W, X and Y.
- He became great American diplomat.
- He used diplomat for American Independence from British.
Having
lived in London for several years and held royal appointments, he instead
pushed for peaceful compromise and preservation of the empire, once by writing “Every encroachment on rights is not worth
a rebellion”. He publicly announced his support for American Independence.
- Continental congress sent him to France to seek military aid for revolution.
Today
there is 1day given to Benjamin Franklin every year Jan 17th in U.
S. A. someone who went to school for 2 years. How many years have you being to
school? At least you can understand me when I say the power of learning.
Other
believers whom I admire includes Isaac Newton and Joseph Hendry
Isaac newton
Throughout
his life, Newton was at pain to prove those mechanistic and naturalistic
philosophers wrong who were attempting to banish God from the universe. He says
“science must be employed to demonstrate
the continuing presence of the creator in the world of Nature”
When
he died his funeral was national event. Quoted in Gale E. Christianson, “In the
presence of the creator”
Joseph Henry
He
says “Men of science – men of God” when
asked to assume a professorship at the University of Pennsylvanian at twice his
government salary, Henry replied simply.
I cannot afford to waste my time in making money showing his devotion to the cause
of science for the benefit of other. He remained in military where God
ordained him. Source: from Cornell University.
According
to Levy Vygostky there are three methods of learning; Imitative, instructed and
collaborative, here I will recommended collaborative learning. Collaborative
learning happen when a peer groups cooperated to learn or achieve a special
goal while working to understand one another, e.g. Projects, group assignment
etc.
Remember
that no one knows all. Sir Isaac Newton once said that “If I have seen any
further, it’s because I stood on the shoulder of giants ahead of me”.
Rub
your mind with sharper mind. The Bible says that “Iron sharpen iron; so a man
sharpens the countenance of his friend. (Prov 27:17).
For
example let’s say I know ¼ and suppose I learn ¼ from other three different
people, then it will make me to know 1. That is wisdom. Remember the definition
of Thomas Edison the inventor of an electric bulb about Genius he says that Genius is someone who is 1% inspiration and
99% perspiration. That means knowledge is acquired not imparted. Therefore
seek for knowledge. Good things do not happen by their own. Good things are
made to happen. (John F. Kennedy).
My
dear listeners I have been speaking so much about the power of learning, the
time will not enough me to speak everything but take time to apply what you
have learned. That is virtue
Remember
the definition of Jesus about Wisdom: Jesus says “Whosoever hears these
sayings of mine and does them, I will liken him to a wise man, which build his
house upon a rock. (Math 7:24-27).
Therefore
wisdom is the acquisition and intelligible application of relevant knowledge
“I,
Jesus, have sent my angel to give you this testimony for the churches. I am the
Root and the offspring of David, and the bright Morning STAR” (Rev 22:16; Holy Bible).
If Jesus is the star, then you are also a STAR.
Apply this knowledge and I see you emerging a STAR in
Jesus name!
Thank you for listening.
UJUMBE : UHUSIANO ULIOPO BAINA YA NDOA NA UFALME WA MUNGU
UTANGULIZI:
Waefeso 5:25-33, Mithali 31:1-31, Ebrania 3:12-14, Mwanzo 24:1-66
Katika
mistari hii utajifunza sifa za mwanamke anayefaa kuitunza na kuilea familia
yake vizuri na kusababisha sifa njema kwa mume wake na watoto wake, mke ambaye
ni mcha Mungu na anaipenda familia yake. Pia utajifunza kwamba mwanaume na
mwanamke watawaacha wazazi wao nao wataambatana pamoja nao wawili watakuwa
mwili mmoja, hii ina maana kwamba wataanzisha familia (ndoa). Mithali 31:1-11 mama yake mfalme Lemueli anamwasa mwanae kwamba
atafute mke mwema kwani yeye ni Mnadhiri wa Bwana.
Katika
kitabu hiki cha Mwanzo wakati Ibrahim
anamwagiza mtumishi wake kwenda kumtafutia mwanae mke kuna mambo ya msingi
alimwagiza azingatie ili mwanae awe na ndoa nzuri.
1.Mwanzo 24:4 maandiko yanasema “bali
enenda hata nchi yangu,na kwa jamaa zangu,ukamtwalie mwanangu Isaka mke”
alimruhusu amtafutie mwanae mke kwa jamii ya watu wake tu ambapo kwa nyakati za
leo tunaweza kusema kijana aliyeokoka anapaswa kuoa mke wa jamii ya wanawake
waliookoka tu.
2.Ibrahimu
alimwambia mtumishi wake kwamba Mungu atampelekea Malaika wake mbele ya
mtumishi wakati anaenda kumtwalia Isaka mke, hii ikiwa na maana ya kwamba Mungu
atakuwa pamoja nae. Hivyo mtumishi wa Ibrahimu alimtanguliza Mungu katika
safari yake ya kumtafuta mke wa Isaka miongoni mwa mabinti wengi wa jamii ya
babaye, kwani si kila binti wa jamii ya babaye alifaa kuwa mke wa Isaka. Mungu
alikuwa ameshamwandalia tayari mke wake.
3.Mke
wa Isaka alifanyika faraja kubwa sana kwa mumewe kwani ile nafasi ya mamae
kwani alikuwa ameshafariki, lakini pia Isaka nae alimpenda sana mke wake nao
wakayatimiza mapenzi ya Mungu yaliyokuwa yamekusudiwa kwao.
Zingatia: Si kila binti
unaemwona machoni pako anafaa kuwa mkeo na si kila kijana unaemwona anafaa kuwa
mume wako kwani jiulize kwanini mtumishi wa Ibrahim asingemchukua yeyote tu
maadam ni jamii hiyohiyo? Kuna mtu mwingine huwezi kuishi nae na kumvumilia
hivyo waachie wenye uvumilivu waishi nao. Hivyo katika somo hili utajifunza ni
jinsi gani ndoa inaweza kuwa na msaada kwako kuuona au kuukosa ufalme waMungu
na changamoto zilizopo katika ndoa zinazowafanya wanandoa kupata shida kwa
habari ya ufalme waMungu.
Swali:
1.
Ni changamoto zipi zinazowapata wanandoa
kuhusu ufalme wa Mungu?
(i)
kusahau huduma au karama ambayo Mungu
ameiweka ndani ya kila mtu ili kusudi kazi yake ijengwe, waefeso 4:11, waefeso
4:7-8
(ii)
kupata ndoa ambayo wanandoa miongoni au mmoja wao hawezi kuibeba huduma au
karama ya mwenzie na kuifanya ikue, hivyo hatari ni hii kuna mtu ukiungana nae
ghafla huduma uliyopewa na Mungu inapotea.
Mithali 31: 30, Mithali 31:10-11, 1Timotheo
4:11-16
(iii)
Kukosa moyo wa msamaha miongoni mwa
wanandoa. Unapokuwa katika ndoa lazima ufahamu kwamba
mume au mke uliyenae siyo Mungu kwamba amekamilika hawezi kusababisha makwazo,
kuna wakati mtapishana katika baadhi ya mambo hivyo moyo wa msamaha unahitajika
kwa kiwango kikubwa sana, msikawie kupeana msamaha kwani haijulikani Bwana Yesu
atarudi wakati gani, yawezekana muda mmekwazana ndo huo huo unyakuo unafika, Mathayo 6:14-15.
(iv) Kukosa moyo wa utoaji miongoni mwao. Changamoto hii ni kubwa sana katika ndoa, kwa mfano unaweza ukawakuta wanandoa baba akawa anapenda sana kumtolea Mungu ila mke akawa na roho ya uchoyo ni mgumu wa kutoa, hii ndoa itakuwa na shida sana kwani kuna wakati baba atatamani kuwakaribisha wageni nyumbani lakini akimwangalia mke wake hapendi wageni. Lakini pia kuna kumtolea Mungu ;
-sadaka -zaka
-malimbuko - shukurani
Kuwasaidia
wasiojiweza n.k, Ayubu 1:1-5, 1Timotheo 6:17-19, 2wakorintho
9:6-8
(vi)
Changamoto nyingine ni wanandoa
kutofahamu kwamba ndoa ni mpango kamili
wa Mungu na Mungu alimuumba mwanamke kwa
ajili ya kumkamilisha mwanaume na
kumsaidia kuyatimiza yaliyo mapenzi ya Mungu.
Changamoto
hii imewaathiri watu wengi kwani walipoingia katika ndoa wakajua ni kuzaa
watoto tu na kuwatunza, wakasahau kwamba kupitia ndoa inapaswa wayatimize
mapenzi ya Mungu. Mwanaume lazima ujue kwamba Mungu amekuletea mke ili
akusaidie kuyatimiza mapenzi ya Mungu wako Mwanzo 1;26-27, Waefeso 5:25-33
(v)
Umaskini. Umaskini umekuwa changamoto kubwa sana kwa kanisa na kusababisha hata
ugumu wa huduma na kuwafanya watumishi wengi kufanya huduma chini ya kiwango
ambacho Bwana anataka afanye na hii imepelekea watu wengi kutotulia makanisani
mwao wakidhani kuhama makanisa kutawasaidia na mwisho wake imekuwa ni
maangamizo. Hivyo umaskini haupaswi kwani ukiwa maskini katika ndoa dhambi haikwepeki
,2Wathesalonike 3:6-1 1Wathesalonike
4:9-12.
(vi) Kutojua kwamba yuko adui ambaye hapendi ndoa
yao ifanikiwe. Mara nyingi watu wengi huwa waaminifu katika kuomba wakati wako
katika uchumba na wakishaingia katika ndoa husahau kwamba bado kuna vita
inapaswa waendelee kuiombea ndoa yao kwa ajili ya ulinzi wao na watoto pamoja
na mali zao, hivyo hujikuta wapo katika matatizo ambayo hayaishi na kusababisha
ugumu hata kwa utumishi waliopewa na Mungu.
(vii) Utofauti wa viwango vya kiroho; Ni vizuri
sana unapomwomba Mungu akupe mwenza wa maisha yako lazima uzingatie huduma
iliyo ndani yako. Kwani viwango vya kiroho ndicho kipimo cha majaribu aliyo
nayo mtu, hivyo ukiambatana na mtu ambaye hana uwezo wa kuibeba huduma yako
fahamu kwamba utashuka viwango vya huduma.
Swali 2: Je ndoa inaweza kuwa fursa ya Shetani kusababisha watu
kutokwenda Mbinguni?
Ni kweli
ndoa inaweza kuwa
ni nafasi ya Shetani kumkosesha mtu katika ufalme wa Mungu pale ambapo watashindwa kutambua changamoto atakazokutana nazo katika ndoa na kukosa hekima ya
kuzitatua. Kumbuka siku zote Shetani hutumia udhaifu wa
mwanadamu kumwangamiza, hivyo
changamoyo hizo zinaweza kufanya adui apate nafasi ya kuwakosesha
katika ufalme wa Mungu Matendo 5:1-11.
Anania
na mkewe Safira walishirikiana kumwibia Mungu na hatima yake wote wakafa
miguuni pa mitume, hivyo inafaa wandoa wajue kushauriana kwa mambo yaliyo mema
machoni pa Bwana.
Zingatia; -Shetani anatumia ndoa kama fursa ya
kuwakosesha watu katika ufalme
wa Mungu
-Ndoa
inaweza kuwa mchango wa kuuwa kipawa cha mtu kama hataungana na mtu mwenye
kusababisha au chochea kipawa chake.
Ndoa
iwe
ni fursa ya kuuona ufalme wa Mungu na sio umeokoka
vizuri halafu baada ya kuingia
kwenye ndoa tu wokovu nao
unapotea. Zingatia utakatifu siku
zote katika ndoa;
Muwe
na kiasi katika mawala ya ndoa
ili msije mpa
shetani nafasi.
Muwe na muda wa kuomba na kusoma neno na wala sio kufurahia ndoa tu huku mkila na
kunywa siku zote.
Fanyeni kila
jambo kwa amani na
upendo huku mkijua kwamba ndoa nayo
ni huduma pia na inapaswa iwe na
utukufu mbele za Mungu.
Wape
ndeni ndugu zenu na kuwasaidia pale walipo na uhitaji kwa
kadri ya uwezo mliojaliwa na Mungu,msiwe
na upendeleo kwa upande mmoja wa ndugu bali watendeeni
pande zote kwa moyo safi.
Muwe na tabia ya kutakiana mema kati yenu mkiwa
katika ndoa (Mithali 15:4).
Fahamianeni
kati yenu na mjue jinsi ya kuchukuliana
madhaifu mliyo nayo
ili shetani asije akapata nafasi
ya kuwakosesha katika Ufalme wa Mungu.
Mpendane,
hurumianeni, sameheaneni, na
mlivyo navyo msinie makuu kupita uwezo wenu, pia msiige namna ya maisha
ambayo ndoa zingine wanaishi, bali muishi kwa kadri mlivyojaliwa, vumilianeni,
muombeane, mheshiniane na kuthaminiana.
Tafuteni
kuwa na familia bora inayompenda Mungu
na kumtumikia kwa moyo safi, pia
fahamuni kwamba huyo mke/ mme uliyenae siyo Mungu, hivyo hajakamilika, kwa hiyo
kuna wakati atasababisha makwazo, lakini neno msamaha lisiondoke
kinywani mwako wakati wote.
Tambueni
ni nini yaliyo mapenzi ya Mungu kwenu na
mtafute kufanya hayo pia jua lisichwe ndani yenu kukiwa
na machungu, msihifadhi neno
la uchungu mioyoni mwenu Shetani
asije akapata nafasi ya kuwamaliza kwa dhambi hiyo.
Tambueni
kwamba kanisa linawategemea, Taifa na jamii kwa ujumla,
hivyo mfahamu na kuwajibika katika nafasi
zenu, msiwe watu wa kupenda pesa
sana msije mkajaribiwa kwa hilo bali ridhikeni na mlivyojaliwa na Mungu.
Zingatia;
Ukiingia au kama uko katika ndoa tambua
kwamba una talanta uliyopewa na Bwana wako ili upate
kumzalishia, talanta inaweza
kuwa ni kipawa, karama au huduma
uliyopewa na Mungu ambayo
ameiweka ndani yako, usishughulikie sana ndoa nayo ikanyamazisha huduma ya
Rroho Mtakatifu ndani yako, bali hakikisheni huduma
zenu zinakua na kumzalia Mungu matunda siku zote. 1Korintho 10:23-33
Swali 3: Je
nini mchango wa ndoa kwa habari ya Ufalme wa Mungu? Isaya 51:1-23
-
Kanisa limeamuriwa kupendana na huku ndiko
kunakopelekea wanandoa kumtumikia Mungu na
kumjengea Ufalme . Yohana 3: 18 Yakobo 1:22
-
Ndoa ni kanisa la Mungu hivyo inapaswa
kumwabudu Mungu na kumtumikia pamoja na
kumfanyia Mungu ibada.
-
Kupitia ndoa
wanazaliwa watoto ambao wanapaswa kulibeba kusudi la Mungu na
kujenga ufalme wake.
Je
wewe unategemea kuwa na
ndoa ya namna gani? Zaburi
127: 1-5 Zaburi 112:1-3, Mithali 15:4
Kwa ulimi
wako unaweza kufanya ndoa yako
ikawa ya baraka na si kuvunja moyo
wengine. Pia tambua kwamba Mungu ndiye
mwenye kuijenga ndoa yenu na kuilinda
ili muweze kumzalia Mungu matunda,
Zaburi 128: 1-6.
Ndoa
njema ni ile ya watu wanaomcha Mungu na kuwa waaminifu kwake kwa habari ya Utumishi.
Mithali 31:1-3, Mithali 12:4, 1korintho 11:7.
MUNGU AKUBARIKI WAKATI UNAPOSOMA NA
KUYAELEWA YALIYOANDIKWA HUMU.
AMENI.
5/06/2016
UJUMBE: JITIE NGUVU
MAANA IMEPASA KUWA HIVYO.
Luka 13:23-24, 18:-30.
War 12:1-2
-Mtu
akikubali kuwa chini ya ufalme Fulani sharti akubali masharti na kanuni
pamoja na sheria zilizo wekwa katika
ufalme huo.
Dhabihu ni sadaka ya shukurani
anayoitoa mtu kwa hiari mbele za Mungu baada ya kutendewa jambo fulani, hivyo Mungu anataka tuitoe miili yetu kuwa
dhabihu hai.
(i)Takatifu-mwli uliotakaswa kwa
kusamehewa dhambi na kuicha kabisa.
-Kwakuwa
Mungu hupenda mahali patakatifu sharti amtume Roho wake Mtakatifu kuja kukaa
katika mwili huo.
Kufuatisha namna ya dunia hii:
Efes 4:17-24
-Kufanya
matendo mfano wa watu ambao hawajaokoka (watu ambao hawaja tolewa kutoka kwenye
ufalme wa giza), watu wanaofanya matendo ya giza, ambao Biblia ina wataja
kwamba niwana wa Ibilisi.
-Watu
ambao fahamu (nia) zao zimetiwa giza hata wasijue ni nini yaliyo mapenzi ya Mungu
anataka nini kwao.
Kolosai 2:4-6,7
-Kinacho
paswa ni kufanya kile ambacho tunajifunza kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwani
yeye anataka tufuate nyayo(yaani matendo aliyo yatenda akiwa duniani).
1. Petro
2:1-2
1. Petro
2:11-12
-kama
watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate
kuukulia wokovu.
·
Maziwa yasiyoghoshiwa ni neno la Mungu
ambalo halijachanganywa na
uongo(chachu) yeyote.
Mfano:
Mtoto mdogo anapozaliwa huanza
kunyonyeshwa maziwa ya mama ambayo humfanya akue na kuwa na afya njema. Lakini mtoto ambaye
hapewi chakula kizuri kinachomfaa mara
nyingi hupatwa na magonjwa kama vile kiriba tumbo, unyafunzi utapiamlo n.k.
1Petro 2:11-2
-Katika
mistari hii inazungumzia kuziepuka tamaa za mwili zipinganazo na roho.
Galatia 5:17
24
Mwili
hutamani ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili, kwa maana hizi
zimepigana hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Warumi 13:11-14
Mwili
unaishi kwa kitambo tu na baada ya muda fulani
huweza kurudi udongoni lakini roho haifi
bali itaishi milele, je ni mahali gani?
Kuna
maneno mawili tu ambayo mtu anapoondoka duniani huweza kuishi ambayo ni;
(i)
Mbinguni
(ii)
Jehanamu
Biblia
inataja Mbinguni kama eneo ambalo wanaostahili kuingia ni wale tu ambao majina
yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo wa Mungu.
Ufunuo 21:1-
Pia
kwa habari ya jehanam ni eneo ambalo wataishi wale wote wote wanaomkataa na
kupinga habari ya neema ya wokovu ambayo imeletwa na mwana wa Mungu Yesu Kristo
ambaye alikubali kuteseka na kujitoa mwili wake kuwa dhabihu kwa dhambi za
wanadamu.
2Korintho 5:22
1Petro 2:22-24
Mathayo 1:21
Hivyo
mtu yeyote anapokufa bila kumwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha
yake na kuhitaji msamaha wa dhambi na kuishi maisha matakatifu ya kumpendeza
Mungu ambayo ni njia ya mtu kuingia katika hii Mbingu.
Hivyo mtu anayeishi kwa kuzifuata tama za
mwili ataiangamiza roho yake kwenda motoni kwani apandacho mtu ndicho atakacho
vuna.
Hivyo imewapaswa kuishi kwa kumtegemea
Roho Mtakatifu na wala si mwili kwani nia ya roho imebeba uzima, bali nia ya mwili ni uangamivu.
Tamaa
za mwili zipiganazo na roho ndicho kikwazo kikubwa cha kuwafanya watu washindwe
kufanya maisha yao kuwa ya utukufu mbele
za Mungu.
Yoh 4:24
Luka 9:23-25
Hivyo
mtu yeyote akitaka kumfuata Yesu na
ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku amfuate.
·
Msalaba unao zungumziwa hapa
ni gharama anayotumia mtu katika
maisha ya wokovu kwa kukubali kupata hasara kwa mambo ya dunia kwani
kuubeba ni gharama kubwa
hivyo imepaswa mtu ajikane mwenyewe ili kuiponya nafsi yake.
Luka 14:27-33
Zab
39:12
Lakini
walio wa kristo wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake
1 Petro 2:24-25
-Mwangalizi
wa roho zetu ni Yesu
Mtu asipotaka kupata hasara kwa vitu vya
duniani hafai katika ufalme wa Mungu.
Math 13:24-30
Mtu
anapobeba kitu chenye heshima inapaswa naye
awe na heshima na bila kikwazo chochote anakuwa na heshima.
Mfano;
Mwanapunda
alipombeba Bwana Yesu kwenda Jerusalemu alikuwa ni mwanadamu ambae bado
hajachoka, bali ndio kwanza anapendeza na anaheshima. Hivyo mwanapunda
alipombeba Bwana Yesu alipata heshima kubwa sana.
Hivyo
aliye mbeba mwenye heshima nae hupata heshima, hivyo kwasababu tumembeba Mungu
mwenyewe heshima inapaswa nasi tuwe na heshima.
MWISHO;
Ili
mtu aweze kubadilika toka katika hali ya udhaifu (dhambi) ni lazima akubali
kupokea neno na kulitendea kazi, kwani wokovu haubadilishwi na mazingira
wala utandawazi.
Ebrania 13:8
Yesu
Kristo ni yeye Yule Jana, Leo na hata Milele------
Habadiliki
na mfano wake haubadiliki.
UBARIKIWE NA BWANA WEWE USOMAYE
NA KUELEWA SOMO HILI: BY EV.NGILIULE NEEMA:Kwa maswali yeyote,
mawasiliano:0767731347,0685630115.
0 comments:
Post a Comment