MAHUBIRI NA MAFUNDISHO

Sunday, 12 February 2017

KUOKOKA-KIPEPERUSHI KILICHOANDALIWA KWA AJILI YA USHUDIAJI.

1.      MAANA YA KUOKOKA
Kuokoka ni kitendo cha kuzaliwa m
ara ya pili yaani kuzaliwa kwa roho.
YOHANA 1:12-13 “ bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Ndio wale waliaminio jina lake(YESU). Wamezaliwa si kwa damu(ukoo), si kwa mapenzi ya mwili wala kwa mapenzi ya mtu(vikao) bali kwa mapenzi ya Mungu.

Wokovu ni neema na mapenzi ya Mungu tu na si vinginevyo, si kwa ajili ya kumfurahisha aliye kushuhudia neno, mhubiri, mzazi, dhehebu, dini au kabila Fulani.

WAEFESO 2 : 8, 9 “kwa maana mmeokolewa kwa neeema kwa njia ya imani ambayo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa(uwezoau nguvu )  cha Mungu. Msitari wa tisa(9) “ si kwa matendo (wema au uzuri au elimu au mali au kimo chako ) mtu awaye yote asije akajisifu” yaani asiwe na kiburi kwa sababu AMEOKOKA.

Kuokoka ni kupata sifa ya kuingia katika ufalme wa Mungu. YOHANA 3: 5-6 “mtu asipozaliwa kwa maji(ubatizo wa maji mengi) na kwa ROHO(IMANI) hawezi kuingia katika ufalme w Mungu.

KUOKOKA ni kufanywa upya baada ya kuuvua utu wa kale au mwenendo( tabia) WAEFESO 4:22-24 ‘vueni kwa habari ya mwenndo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kuzifuata tama zidanganyazo mfanywe upya, mkavae utu upya ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

2.      HATUA MBILI ZA KUCHUKUA WAKATI WA KUOKOKA
WARUMI 10: 9-10
(i)                 KUKIRI;- Ukimkiri(kutamka) kwa kinywa chako yakuwa YESU kristo ni  BWANA  na mwokozi wa maisha yako UTAOKOKA.
(ii)               KUAMINI;- Ukiamini kuwa MUNGU alimleta yesu duniani akazaliwa, akafa kwa ajili ya dhambi zako na akafufuka kutoka katika wafu UTAOKOKA.
3.      KWA NINI TUNAOKOLEWA KWA NJIA YA IMANI?
(I)                 Kwa sababu lazima ubadili imani yako iliyojengwa katika mizimu, uganga, upagani, uchawi, uisramu, matambiko, kafara n.k. sas umwamini MUNGU wa miungu na Bwana wa mabwana ambaye imani ktika yeye imejengw katika neno lake . WARUMI 10:17- “basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo(YESU)
(II)              Kwa sababu pasipo imani haiwezekani kumpendeza MUNGU,
WAEBRANIA 11:6 –“ pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila amwendeaye(anyetaka kuwa mtoto MUNGU) lazima aamini ya kwamba MUNGU yupo na kwamba huwapa thawabu(Baraka, kibali, majibu) wale wamtafutao”
4.      MAMBO MHIMU YA KKUZINGATIA BAADA YA KUOKOKA.
(a)                Wokovu unapatikana kwa YESU pekee, si katika dini au mtume au nabii au dhehebu lolote. Usianganyike.
 MATENDO 4:12. Toba ndio njia pekee yakumrud ia na  kutengeneza na MUNGU na kutafuta amani. MATENDO 3:19, 1YOHANA 1:8-9( kwa toba tunapata ondoleo la dhambi)
(b)               Epuka tama zipinganazo na roho na jitahidi kutenda mema. 1PETRO 2 : 11-12, zingatia sana YAKOBO 4: 17  biblia inasema “ yeye ajuaye kutanda mema na  wala hayatendi kwake huyo ni dhambi”.
(c)                Mtii MUNGU daima na mpinge shetani mara zote yeye pamoja na ushawishi wake wote. YAKOBO 4:7 “ basi mtiini MUNGU mpingeni shetani, mkalibieni MUNGU nae atawakaribia ninyi.
(d)               Kaa ndani ya YESU ili upate kuzaa sana, kustawi, kufanikiwa. YOHANA 15:1-17.
(e)                Tafuta kanisa la watu waliookoka ili ukamwabudu MUNGU  huko, ili ukue kuroho. MATENDO 2:4-42
ishi kwa kumaanisha maisha ya wokovu(kubali kubadilika, kubali kubatizwa na kujifunza neno ili uwe mwanafunzi wa yesu. MATHAYO 28:19-20.

SALA YA TOBA
 “BWANA YESU nakiri mimi ni mwenye dhambi, naomba unisamehe dhambi zote nilizozitenda kwanza kwa maneno na kwa matendo unitakase kwa damu yako, karibu moyoni mwangu, uwe BWANA NA MWOKOZI  wa maisha yangu, naomba ufute jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima, wewe shetani kuanzia leo! Ninakukataa na kazi zako zote, BWANA YESU naomba ROHO mtakatfu anisaidie kuishi maisha matakatifu, kwa jina la YESU Kristo naamini NIMEOKOKA AMENI!




posted by MR. BOAZ ELIYA,
edited by evanglism departiment 
cooperating with EV.  DASTAN 

0 comments: