Harakati za kuanza kwa CASFETA
zimekuwepo tangu mwaka 1984.Wakati huo Mch. JOSEPH JUSTINE alianza
huduma kwa wanafunzi kama kuitikia wito wa kumtumikia Mungu, Kwa
watoto na vijana hasa wa shuleni na vyuoni. Kwanza aliunda jumuiya
aliyoiita “The Teenegers Bible Clubs”(TBC), ambayo iliwajumuisha
wanafunzi wa shule za msingi. Mwaka 1986, Mch. J. Justine kwa
ushirikiano na baadhi ya wanafunzi waliookoka mkoani DAR ES SALAAM
walianzisha “THE Dar es salaam Inter Secondary Christian Students
Fellowhip” (DISCF). Kwa kipindi cha kuanzia 1980-1992 vilianzishwa
vikundi mbalimbali vya wanafunzi mikoani vya kipentekoste kwa lengo
la kuwaunganisha. Kilimanjaro kulikuwa na kikundi kilichoitwa KISA,
Singida kiliitwa CAF, Tanga kiliitwa “GOSPEL ARMY”, Ruvuma CA na
Arusha kulikua na huduma iliyoitwa “THE POWER GOSPEL TEAM”
ambayo ilikuwa na idara ya Huduma kwa wanafunzi.
Haja ya kuwa na umoja wa
wanafunzi wa kipentekoste (Pentecostals) ya kitaifa ilikuwepo na
ilijadiliwa na watu mbalimbali. Mchungaji Joseph Justine aliamua
kuitendea kazi (1987). Alitengeneza Mpango Pendekezo (Proposal) na
Katiba ya Awali.
Pia alitafuta ushirikiano na
kutaka kuungwa mkono na watu wengine na wachungaji. Hao ni pamoja na
Mchungaji John Senyagwa(1987,KLPT), Mchungaji Andrew Mwenibungu
(1988,HOLINESS) , Mchungaji Titus Mkama (1990-1992,TAG) Ndugu Oddo
Egino Hekela (Rais Mteule wa CASFETA,1992/1993) Ndugu Emanuel Akili
(Katibu Mkuu wa kwanza wa CASFETA) na Ndugu Juliasi E Mkenda,
(1993,TAG). Juhudi hizi ziliendeshwa kwa pamoja na wanachama
waanzilishi wa CASFETA, mwaka 1992. Mkutano wa kwanza wa kutangaza na
kuanzisha CASFETA ulifanyika tarehe 25/06/1992 katika chuo cha
uhasibu Dar es salaam na ulihudhuriwa na wanafunzi 72 ambao wote
walikubali kuwa wanachama wa CASFETA.
Maazimio ya kudumu ya CASFETA
- CASFETA ni umoja wa wanafunzi wa kikristo wa aina ya Kipentekoste. Popote CASFETA ilipo izingatie misingi ya Imani ya Kipentekoste.
- CASFETA izingatie daima umoja wa kweli katika Kristo mahali popote (Ef. 4;1-5)
- Heshima ni kitu kinachozingatiwa sana katika CASFETA hasa kwa kuzingatia kwamba wanachama katika CASFETA ni vijana. Wanapaswa KUHESHIMU na kuwajibika kwa wakubwa.
- Neno la Mungu, yaani Biblia ndio Msingi Mkuu wa CASFETA. Wanachama na viongozi wote wanatakiwa wasome na kuelewa Biblia na kufuata maelekezo yake.
- Elimu (Secular education ) ni jambo linalotiliwa mkazo mkazo katika CASFETA. Wanachama na viongozi wote katika CASFETA wanatakiwa wawe na bidii katika kusoma ili wafaulu vizuri mitihani yao.
Mambo makuu matatu ya
kuzingatia
1) Umoja
2) Utakatifu na
3) Elimu.
Sifa za mwanachama
- Awe mkristo aliyezaliwa mara ya pili (Aliyeokoka).
- Awe ni mwanafunzi katika shule,chuo/chuo kikuu kwenye tawi husika.
- Awe mshirika mwaminifu katika kanisa lake analoshiriki (local congregation).
- Awe amebatizwa katika ubatizo wa Kipentekoste, yaani wa maji tele na kujazwa roho mtakatifu, kwa ishara ya kunena kwa lugha na awe na maisha safi yenye ushuhuda wa Kristo.
Kupoteza au kumaliza
uanachama
- Hatatekelezai madhumuni ya chama, au kuhudumu katika masharti ya uanachama.
- Amemaliza muda wake wa uanafuzi. Baada ya mwanaCASFETA kumaliza elimu yake atakuwa ni mhudumu katika TAYOMI.
- Kama amefariki.
- Mwanachama akipoteza uanachama hatakuwa na haki ya kudai chochote.
0 comments:
Post a Comment