CASFETA-TAYOMI-SJUT-DODOMA

CHRIST AMBASSADORS STUDENTS FELLOWSHIP - TANZANIA YOUTH MINISTRY - ST JOHN'S UNIVERSITY OF TANZANIA.

UMOJA, UTAKATIFU, ELIMU

TO CHANGE THE LIFE OF THE YOUTH, TO CHANGE THE WORLD.

CHOOSEN GENERATION BAND SJUT DODOMA

YOU CAN DO EVERYTHING THROUGH CHRIST WHO GIVES YOU STRENGTH....PHILLIPPIANS 4:13.

CASFETA TAYOMI SJUT

"SO DO NOT FEAR, FOR I AM WITH YOU, DO NOT BE DISMAYED, FOR I AM YOUR GOD, I WILL STRENGTHEN YOU AND HELP YOU, I WILL UPHOLD YOU WITH MY RIGHTEOUS RIGHT HAND"....Isaiah 41:10.

INREACH DODOMA

THE PREACHING OF CHRIST IS THE WHIP THAT FLOGS THE DEVIL, THE PREACHING of CHRIST IS THE THUNDERBOLT, THE SOUND OF WHICH MAKES HELL SHAKE.

MAHUBIRI NA MAFUNDISHO

Tuesday 14 February 2017

UCHUMI NA MKRISTO by ALEX JOHN WAMBI. MWALIMU WA FPCT CHAMWINO DODOMA.

UCHUMI NA MKRISTO
 SI MAPENZI YA MUNGU TUWE NA MAISHA DUNI/ MASKINI
 Napenda kuanza kukuambia ya kuwa si mapenzi ya Mungu uwe maskini. Kwa sababu tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu huu, Mungu hakupanga kuwa watu wake aliowaumba wawe maskini; bila kujali rangi, kabila, wala taifa. ( Kumbuka EFESO 3:20;)
 Mtu maskini maana yake ni mtu mhitaji. Mtu aliye maskini wa mambo ya mwili ni yule aliye mhitaji wa mambo ya mwili. Na mambo ya mwilini ninayoyasema ni mavazi, chakula na mahali pa kulala. Yesu Kristo hakusema heri wale walio na mahitaji ya chakula, mavazi, afya na malazi.
Japo ni  imeandikwa katika Mithali 22:2, kuwa “Tajiri na maskini hukutana pamoja; Bwana ndiye aliyewaumba wote”. Lakini fahamu ya kuwa ingawa matajiri na maskini waliopo wote waliumbwa na Mungu; tangu mwanzo wa uumbaji Mungu hakuyaweka matabaka haya mawili.
 SABABU 4 KWA NINI SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASIKINI.
  1. Mungu ndiye atupaye nguvu za kupata utajiri
“ Bali utamkumbuka Bwana , Mungu wako, maana ndiye akupaye NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo” (Kumb. 8:18).
Lakini fahamu ya kuwa si matajiri wote waliopo duniani wameupata utajiri kutokana na nguvu walizopewa na Mungu. Wengi wamepata utajiri kwa njia ya dhuluma. Na ndiyo maana sehemu nyingi katika Biblia matajiri wa jinsi hiyo wamekemewa. Soma Amosi 5:11, 12. Kwa sababu hii Mungu hayuko upande wa matajiri hawa. Hii pia haimaanishi kuwa Mungu yuko upande wa KILA  maskini aliopo duniani. La hasha! Mungu yuko upande wa yule ayafanyaye mapenzi yake awe tajiri au maskini (Mathayo 7:21)
  1. Mungu ndiye atufundishaye kupata faida
Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo Yesu si Mungu wa hasara bali Mungu wa faida. Imeandikwa hivi;  “ Bwana, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi;Mimi ni Bwana, Mungu wako,   nikufundishaye  ili upate faida, nikuongozaye katika njia  ikupasayo kuifuata” (Isaya 48:17).
  1. Vitu vyote vyema ni mali ya Bwana, na vyote vya Bwana ni vyetu ndani ya Kristo
              Katika Zaburi 24:1 imeandikwa;“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana; Dunia na wote wakaao ndani yake”
            Na pia ukisoma katika Hagai 2:8 unaona imeandikwa hivi “Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi”

  1. Yesu Kristo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri
              “ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi   alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” (2 Wakorintho 8:9).          
            Je! unafahamu kwa nini Yesu Kristo aliamua kuwa maskini? Ni “…….. ili kwamba ninyi mpate kuwa MATAJIRI kwa umaskini wake”.
           Najua kuna wengine watashangaa kuusoma mstari huu; lakini ndivyo ilivyo. YESU ansema Na ndiyo maana alisema katika Luka 4:18a ya kuwa; “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri MASKINI habari njema.”
Mtume Petro naye aliwahi kusumbuliwa sana na jambo hili, hata ikabidi amuulize Bwana Yesu.
        “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata, TUTAPATA NINI BASI?” (Mathayo 19:27)
          “Yesu akasema, Amini, nawaambiaeni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa MARA MIA SASA WAKATI HUU, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele” (Marko 10:29,30).
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ……." (Hosea 4:6). Maneno haya yaliyosemwa na Mungu kwa kinywa cha Nabii Hosea yana ukweli ndani yake hata hivi leo. Watu wengi sana siku hizi wanaangamizwa, wanadhulumiwa, wanahuzunishwa na maisha kwa sababu tu wamekosa kuyajua maarifa ya Mungu yaliyomo katika Neno lake.
Tulikuwa tunafurahi tunaposoma mstari kama ufuatao; " …..vyote ni vyenu …. Vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu, nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu" (Wakorintho 3:21,22). Tulikuwa tunafurahi kwa kuwa maneno haya yanatupa uhalali wa kumiliki vitu vilivyo vya Mungu. Kwa mfano Hagai 2:8 inasema "Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa Majeshi." Pia, Zaburi 24:1 inasema "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana …" Lakini jambo lililotusumbua ni kwamba ingawa mistari hiyo ilitupa umilikaji juu ya fedha, dhahabu na vyote viijazavyo nchi ili tuvitumie – SISI HATUKUWA NAVYO WALA HATUKUJUA TUTAVIPATAJE!
Tulitamani sana kuona maneno ya Wafilipi 4:19 yanatimia kwetu – nayo yanasema hivi;
"Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu".
·         Lakini mnaweza kushinda kwa kusimama katika Neno langu ambalo ni upanga wa Roho mikononi mwenu.
·         Nimesema katika Yoshua 1:8 ya kuwa mtafanikiwa ikiwa mambo matatu yatafanyika juu ya Neno langu:

(a) Lisiondoke kinywani mwenu 
(b) Mlitafakari wakati wote
(c) Na kudumu kulitenda

            Ahsante,


KANUNI ZA  USIMAMIZI MZURI WA FEDHA KWA MWAMINI/MKRISTO:
usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako na kuukuza uzalishaji wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini kama una usimamzi mbaya wa fedha  uchumi wako utayumba tu.Matatizo mengi ya kifedha tunakimbilia kuombewa na kukemea,lakini hayo yote bila  kujifunza usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika mzizi.hata ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha matatizo ya kifedha yatarudi baada ya muda mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi kanuni za fedha.


1: JIFUNZE KUWEKA NA KUWEKEZA AKIBA USILE KILA KITU UPATAPO TOKA KWA BWANA!

Kosa Kubwa Wanalofanya Wana Wa Mungu, Hasa Wale Waliookoka, Wanaoishi Kwa Imani, Ni Kutojua Kuwa Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Ndani Ya Muda Maalumu, Na Hurudi Kutupa Tena Baada Ya Muda, Na Sio Kwamba Mungu Huwa Anatoa Mahitaji Yetu Kila Siku… Hii Naizungumzia Kwenye Maeneo Ya Mahitaji Yetu Ya Kifedha, Chakula, Vyakula, Mavazi Nk… Mungu Anapokupa Kitu, Mahitaji Yako, Huwa Anakupa NA ZIADA, Hakupi Kipimo Cha Kula Au Kutumia Muda Ule Tu… Huwa Anatoa NA CHA ZIADA AU NYONGEZA JUU… Lengo Kubwa La Mungu Kukupa KITU CHA ZAIDI AU ZIADA Ni Ili Akusaidie Kwenye KESHO YAKO (Future)… Narudia Tena, Mungu Huwa Anatupa Na Ziada, Lengo Lake Kubwa Ni Kufidia MUDA ULIOPO KATIKATI HAPA Kati Ya Pale Alipokupa Hadi Pale Atakaporudi Tena Kukupatia Tena! MWANZO 41:25-35,48,49.
NDIO MAANA Mungu Anatufundisha Habari Za Chungu, Wasio Na Msimamizi Wala Kiongozi Ambao Wakati Wa MAVUNO Hawali Chakula Chote Bali HUJIWEKEA AKIBA Inayowasaidia Wakati Wa UKAME NA NJAA MITHALI 6:6-8 NA 30:24-25…
Lakini Pia Mara Nyingi Kwenye NENO LAKE, Mungu Amezungumza Kuhusu GHALA… Ambayo Ni Sehemu Ya Kuhifadhia Au Kutunzia MAVUNO/ ULICHOPATA Kwa Ajili Ya KESHO YAKO… Pia Mungu Mara Nyingi Amesema Kuhusu HAZINA… Inayomaanisha SHEHENA ILIYOHIFADHIWA Kwa Ajili Ya MATUMIZI YA BAADAYE… Na Mara Nyingi Mungu Anapokuja KUTUBARIKI, Huwa Analenga HAZINA NA GHALA ZETU… Utamsikia Akisema, “Nipate KUZIJAZA HAZINA NA GHALA ZENU” (Malaki 3:10).

Lakini Hata Yesu Mwenyewe Alijua Kanuni Hii Na Aliitendea Kazi… Hata Wakati Alipowalisha Wale Wanaume 5000, Wanawake Wengi Na Watoto, BADO YEYE NA TIMU YAKE WALIKUSANYA CHAKULA KILICHOBAKI
(Marko 6:42-43, Yohana 6:12-13)
 YESU Alikuwa Na Uelewa Wa Kutosha Kuhusu Mungu, Baba Yake Ya Kuwa Huwa Anatoa ZIADA, Lakini Usipoitunza Na KUTUMIA KILA ULICHOPATA, BILA KUWEKA AKIBA, Kuna Muda Unakuja Ambao Utakuwa Na Uhitaji Na Hata Ukimlilia Na Kumwita Mungu, HATAKUJIBU AU KUKUPA Kingine Mpaka Muda Ule Aliopanga Utakapofika!


Mungu Anapokufungulia MLANGO Wa Kupata MSHAHARA, Au Kipato Kizuri Kwenye Biashara Au Shughuli Zako Za Uzalishaji, USITUMIE KILA ULICHOPATA… JIWEKEE AKIBA… WEKA GHALANI Kwa Ajili Ya Kesho Yako Au Itumie Ile Ziada Kwa Ajili Ya KUZALISHA FAIDA ZAIDI [WEKEZA ILE ZIADA] Kwenye shughuli Au Jambo Litakalokupa Zaidi Ya Ile Na Kukuvusha Kipindi Cha UGUMU Kitakapokuja!

Jifunze Kuweka Akiba… Lakini Mara Baada Ya Kupata Hiyo Akiba, Iwekeze Mahali Ambapo Unaweza Kuiongeza Ili Uwe SALAMA Wakati Wenzako Watakopokuwa WANALIA NJAA


2. TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA NA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA
Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza kukusaidia katika kuandaa bajeti yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari ndogo na anza kuweka kumbukumbu za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini itakusaidi kwa mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa usafiri?simu?chakula?matibabu?chakula n.k ni lazima ujue wapi fedha yako inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina mililki nini, nina nini, nina daiwa,natuamiaje (MITHALI 27:23-24, 23:23,)

3. JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU, KWA NANI NA KWA UTARATIBU.
(Mithali 11:24-25).kanuni ya uchumi wa Kimungu ni tofauti,kadiri unavyotoa na sivyo unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa kwaajili ya kuwabariki wengine,kutoa kwaajili ya wahitaji(Mithali 28:27 Mithali 11:25.Mithali 19:17,Mithali 3:9-10),Kutoa  kunafungua Baraka za Mungu katika Maisha yako.

 (A) tumia fedha yako kwa hekima na ridhika na ulicho nacho:

Zingatia vipaumbele na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila mpangilio,manunuzi ya papo kwa papo,usifanye matumizi yaliyo nje,yanayozidi kipato chako au uwezo wako wa kifedha.Jifunze kuridhika na kuuepuka tamaa.usifuje fedha kwa matumizi ya ovyo.jifunze kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9)



Alex John Wambi,
Mwalim,FPCT Chamwino.

MKUTANO WA IN REACH ST. JOHN UNIVERSITY OF TANZANIA

WANASIFA WAKIMSIFU MUNGU




WATU WALIOAMUA KUMPOKA YESU WAKIOMBEWA SALA YA TOBA.





Sunday 12 February 2017

KUOKOKA-KIPEPERUSHI KILICHOANDALIWA KWA AJILI YA USHUDIAJI.

1.      MAANA YA KUOKOKA
Kuokoka ni kitendo cha kuzaliwa m
ara ya pili yaani kuzaliwa kwa roho.
YOHANA 1:12-13 “ bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Ndio wale waliaminio jina lake(YESU). Wamezaliwa si kwa damu(ukoo), si kwa mapenzi ya mwili wala kwa mapenzi ya mtu(vikao) bali kwa mapenzi ya Mungu.

Wokovu ni neema na mapenzi ya Mungu tu na si vinginevyo, si kwa ajili ya kumfurahisha aliye kushuhudia neno, mhubiri, mzazi, dhehebu, dini au kabila Fulani.

WAEFESO 2 : 8, 9 “kwa maana mmeokolewa kwa neeema kwa njia ya imani ambayo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa(uwezoau nguvu )  cha Mungu. Msitari wa tisa(9) “ si kwa matendo (wema au uzuri au elimu au mali au kimo chako ) mtu awaye yote asije akajisifu” yaani asiwe na kiburi kwa sababu AMEOKOKA.

Kuokoka ni kupata sifa ya kuingia katika ufalme wa Mungu. YOHANA 3: 5-6 “mtu asipozaliwa kwa maji(ubatizo wa maji mengi) na kwa ROHO(IMANI) hawezi kuingia katika ufalme w Mungu.

KUOKOKA ni kufanywa upya baada ya kuuvua utu wa kale au mwenendo( tabia) WAEFESO 4:22-24 ‘vueni kwa habari ya mwenndo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kuzifuata tama zidanganyazo mfanywe upya, mkavae utu upya ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

2.      HATUA MBILI ZA KUCHUKUA WAKATI WA KUOKOKA
WARUMI 10: 9-10
(i)                 KUKIRI;- Ukimkiri(kutamka) kwa kinywa chako yakuwa YESU kristo ni  BWANA  na mwokozi wa maisha yako UTAOKOKA.
(ii)               KUAMINI;- Ukiamini kuwa MUNGU alimleta yesu duniani akazaliwa, akafa kwa ajili ya dhambi zako na akafufuka kutoka katika wafu UTAOKOKA.
3.      KWA NINI TUNAOKOLEWA KWA NJIA YA IMANI?
(I)                 Kwa sababu lazima ubadili imani yako iliyojengwa katika mizimu, uganga, upagani, uchawi, uisramu, matambiko, kafara n.k. sas umwamini MUNGU wa miungu na Bwana wa mabwana ambaye imani ktika yeye imejengw katika neno lake . WARUMI 10:17- “basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo(YESU)
(II)              Kwa sababu pasipo imani haiwezekani kumpendeza MUNGU,
WAEBRANIA 11:6 –“ pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila amwendeaye(anyetaka kuwa mtoto MUNGU) lazima aamini ya kwamba MUNGU yupo na kwamba huwapa thawabu(Baraka, kibali, majibu) wale wamtafutao”
4.      MAMBO MHIMU YA KKUZINGATIA BAADA YA KUOKOKA.
(a)                Wokovu unapatikana kwa YESU pekee, si katika dini au mtume au nabii au dhehebu lolote. Usianganyike.
 MATENDO 4:12. Toba ndio njia pekee yakumrud ia na  kutengeneza na MUNGU na kutafuta amani. MATENDO 3:19, 1YOHANA 1:8-9( kwa toba tunapata ondoleo la dhambi)
(b)               Epuka tama zipinganazo na roho na jitahidi kutenda mema. 1PETRO 2 : 11-12, zingatia sana YAKOBO 4: 17  biblia inasema “ yeye ajuaye kutanda mema na  wala hayatendi kwake huyo ni dhambi”.
(c)                Mtii MUNGU daima na mpinge shetani mara zote yeye pamoja na ushawishi wake wote. YAKOBO 4:7 “ basi mtiini MUNGU mpingeni shetani, mkalibieni MUNGU nae atawakaribia ninyi.
(d)               Kaa ndani ya YESU ili upate kuzaa sana, kustawi, kufanikiwa. YOHANA 15:1-17.
(e)                Tafuta kanisa la watu waliookoka ili ukamwabudu MUNGU  huko, ili ukue kuroho. MATENDO 2:4-42
ishi kwa kumaanisha maisha ya wokovu(kubali kubadilika, kubali kubatizwa na kujifunza neno ili uwe mwanafunzi wa yesu. MATHAYO 28:19-20.

SALA YA TOBA
 “BWANA YESU nakiri mimi ni mwenye dhambi, naomba unisamehe dhambi zote nilizozitenda kwanza kwa maneno na kwa matendo unitakase kwa damu yako, karibu moyoni mwangu, uwe BWANA NA MWOKOZI  wa maisha yangu, naomba ufute jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima, wewe shetani kuanzia leo! Ninakukataa na kazi zako zote, BWANA YESU naomba ROHO mtakatfu anisaidie kuishi maisha matakatifu, kwa jina la YESU Kristo naamini NIMEOKOKA AMENI!




posted by MR. BOAZ ELIYA,
edited by evanglism departiment 
cooperating with EV.  DASTAN 

Wednesday 18 January 2017

SEMINA YA UAMUSHO WA ROHO MTAKATIFU

>>SEMINA>> UAMSHO WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA. NA MWL. ALBERT MWASHAMBWA<<
Uamusho wa roho mtakatifu nini?
contents: 1. Maana ya uamusho wa roho mtakatifu katika kanisa ni nini?
UAMSHO WA ROHO MTAKATIFU; ni hali ya kanisa kuwajibika kulingana na utendaji kazi wa roho mtakatifu au is a state of a church to respond according to holy spirit working. mchanganuo wa maana ya uamsho wa roho mtakatifu.
   hali ni mabadiliko ya mtu ambayo yanaweza kutokeza nje na kuleta matokeo. hali ndio inayoweza kufanya mtu aonekane vile anaonekana, lakini pia hali hufanya matokeo ya maamuzi anyofanya mtu na hi huletw na nguvu au msukumo au nguvu inayofanya maamuzi ndani ya mtu.
   kama tuluvyokwisha kuona kuwa uamusho wa roho mtakatifu nini. tunaweza kusema kuwa ;
UAMUSHO WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KANISA
               2. maana ya uamusho katika maneno "uamusho" 
               3. Roho mtakatifu ni nani?
               4. Roho mtakatifu ni nini juu ya mtu. 
               5. Roho mtakatifu ndani ya mtu ni nini.
               6. Roho mtakatifu kama maji.
               7. Roho mtakatifu kama moto.
               8. tabia za Roho mtakatifu. 
                9.Kazi za Roho mtakatifu.
                10. Wajibu wa kufanya kuwa na Roho mtakatifu.

MKUTANO MKUBWA WA INJILI NA CASFETA TAYOMI SJUT

UPCOMING EVENTS
mkutano huo unafanyikia katika eneo la kanisa la FPCT KIKUYU. Wahubiri katika mkutano huo ni wanacasfeta wenyewe, ambao miongoni mwao ni EV. IISSACK SUDI na EV. ELIYA SAMWELI na EV. HALINGA FAUSTINE.
Wenye shida mbalimbali watafanyiwa maombi na kuponywa kwa jina la YESU KRISTO.
neno la Mungu linasema "Akawaambia enendeni ulimwenguni mwote mukaihubiri injili kwa kila kiumbe. Aaminie na kubatizwa ataokoka asiyeamini atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya.watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha hakita wadhuru kabisa, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya"(marko 16:15-18) 
in english
 He said to them, “Go into all the world and preach the good news to all creation.   Whoever believes and is baptised will be saved, but whoever does not believe will be condemned.  And these signs will accompany those who believe: In my name they will drive out demons; they will speak in new tongues;  they will pick up snakes with their hands; and when they drink deadly poison, it will not hurt them at all; they will place their hands on sick people, and they will get well.”  After the Lord Jesus had spoken to them, he was taken up into heaven and he sat at the right hand of God.  Then the disciples went out and preached everywhere, and   the Lord worked with them and confirmed his word by the signs that accompanied it.(mark 16:115-20)

USHUHUDIAJI KATIKA WIKI YA USHUHUDIAJI TAR. 06-13/01/2017

Ushuhudiaji kama agizo ambalo tumepewa na Mungu. ni sehemu moja wapo ambayo CASFETA-TAYOMI SJUT wanamtumikia mungu kwa njia hiyo. tarehe 6 siku ya jumaosi ya kwanza ya mwaka 2017 ushuhudiaji ulianza katika chuo kuku cha ST. JOHN'S UNIVERSITY OF TANZANI.
Ushuhudiaji huo ulifanyika ndani ya chuo katka madarasa na sehemu wanazoishi wanachuo hao. wako waliofunguliwa na kuponywa siku hiyo pia watu kadha wa kadha walimpokea YESU kuwa BWANA na  mwokozi wa mwokozi wa maisha yao.
hitimisho katika siku hiyo ilifanyikia eneo la mdegree ambapo EV. FAUSTINE HALINGA alihubiri akishirikiana na EV ISSACK SUDI.>>>MAHUBIRI SIKU YA USHUHUDIAJI MDEGREE KATIKA CHUO KIKUU CHA ST. JOHN'S UNVERSITY OF TANZANIA. NA EV. HALINGA FAUSTINE & EV. ISSACK SUDI.



Wednesday 26 October 2016

KARIBUNI FRESHER'S WOTE CASFETA TAYOMI SJUT

Uongozi wa CASFETA TAYOMI SJUT  unapenda kuwakaribisha wanachuo wote walijiunga na mwaka wa masomo 2016/2017na wengineo kwenye ibada zinazofanyia chuoni ST JOHN.CASFETA  TAYOMI inajumuisha wakristo wote wanaotoka makanisa mbalimbali ya kipentekoste nchini Tanzania na hata nje ya nchi mf wa makanisa hayo ni TAG,EAGT,PEFA,WINNERS,PAG,CAG na mengineyo.Hivyo uongozi unapenda kuwakaribisha wanavyuo wote waliojiunga mwaka huu wa masomo kufika katika ibada hizo.
MKARIBISHE NA MWINGINE MUNGU AKUBARIKI

Wednesday 14 September 2016

MKUTANO SIKU YA 3

Nimuendelezo wa mkutano ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano huu unaoendelea hapa LUBAGA-SHINYANGA,Yesu amekuwa akitenda miujiza na ishara mbalimbali na huku tukishuhudia watu wengi wakimpokea YESU kuwa Bwana na Mwokozi wao,Jumla ya watu 315 waliokoka hii ikiwa ni watu 300 walmpokea Yesu kwa njia ya ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba na  watu 15 kwenye mkutano wa jioni.

JUKWAA KABLA YA MKUTANO KUANZA,FUNDI MITAMBO WAKIWEKA MAMBO SAWA

WANACASFETA WAKIMSIFU MUNGU WAKATI WA MKUTANO




KWAYA YA LUBAGA WAKIIMBA


CHOSEN GENERATION BAND WAKIMSIFU MUNGU WAKATI WA MKUTANO


WANACASFETA WAKIMCHEZEA MUNGU

NA WATOTO NAO WALIKUWA WAKIMSIFU MUNGU 


WANACASFETA WAKIJIANDAA KUIMBA WAKATI WA MKUTANO


WAHUDUMU NAO WAKIWA TAYARI KUKUSANYA SADAKA

MWIMJILISTI NEEMA NGILIULE  AKIMHUBIRI YESU

MWINJILISTI NEEMA NGILIULE AKISISITIZA JAMBO

WATU WAKIENDA MBELE KUOMBEWA NA KUMPOKEA YESU KRISTO


WALIOKUWA  WAKIMPOKEA YESU KRISTO WAKIOMBEWA BARAKA NA KUFUNGULIWA  KATIKA VIFUNGO MBALIMBALI




WALIOKUWA  WAKIMPOKEA YESU KRISTO WAKIOMBEWA BARAKA NA KUFUNGULIWA  KATIKA VIFUNGO MBALIMBALI





Tuesday 13 September 2016

MKUTANO MKUBWA WA INJILI SHINYANGA-LUBAGA, NA CASFETA TAYOMI ST JOHN(SJUT)

Mkutano mkubwa wa injili ulioanza tarehe 10-18/09/2016 maeneo ya lubaga shinyanga,Umekuwa wa tofauti na wenye nguvu za Mungu,yafuatayo ni matukio mbalimbali kuanzia  mwanzo wa mkutano na kuendelea hadi mwisho.Ikiwa ni siku ya pili tu ya mkutano jumla ya watu 155 walimpokea YESU hii ikijumuisha mkutano wa mchana,ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba na SINEMA ya usiku 


SIKU YA KWANZA NA YA PILI


Wana ST JOHN  wakiwa ndani ya BASI wakitoka DODOMA kuelekea LUBAGA/SHINYANGA




Mlezi SULEMANI KURWAkushoto akiwa pamoja na mwenyekiti watawi ISACK SUDI,Mwenyekiti mstaafu Patric JOHN CHUWA na wahubiri wengine ,dada NEEMA NGILIULE  na Mwinjilisti ELIYA 




Mwimbaji kutoka UGANDA  Akimsifu MUNGU katika Viwanja vya mkutano IEAGT -LUBAGA SHINYANGA




   Wahudhuriaji wa Mkutano wakifuatilia mkutano kwa Makini


 JC CHOIR wakimsifu Mungu
     IEAGT CHOIR wakimsifu MUNGU katika mkutano


DADA CLENE DOTTO akiendelea na Maombi wakati mkutano ukiendelea
 KWAYA ya CASFETA ST JOHN wakijiandaa kumuimbia MUNGU katiaka mkuano huo



 Wahudumu wamkutano wakiwa mbele ya jukwaa tayari kwa kufanya huduma


 Praise Team wakimwabudu Mungu



MHUBIRI WA MKUTANO mwinjilist ISACK SUDI akiwa tayari kumhubiri YESU KRISTO












Wana SJUT wakiwa na matawi na vuvuzela kwa ajili ya kumshangilia Mungu wakati wa Mahaubiri

WATU wakiwa mbele kwa ajili ya kuombewa




Waongofu waya wakiwa mbele ya mkutano tayari kwa kumpokea YESU KRISTO